Minyoo husababishwa na nini,Minyoo huingiaje mwilini

Minyoo husababishwa na nini,Minyoo huingiaje mwilini

#1

Minyoo husababishwa na nini,Minyoo huingiaje mwilini

Njia ambazo minyoo huweza kuingia mwilini na kukushambulia ni Zipi?

Minyoo kwa binadamu hupatikana kutokana na vyanzo mbalimbali, hasa vinavyohusiana na usafi duni na mazingira.

Article author: Dr.Ombeni Mkumbwa
Reviewed: Afyaclass, MD's

Kwanini Unasikia Meza dawa za Minyoo Kila baada ya miezi 3, Miezi 6 na kuendelea hata kama huoni dalili zozote. Hii inatokana na Mazingira mengi tunayoishi yanakuwa na Kiwango kikubwa cha Minyoo hali ambayo hupelekea watu wengi kuipata bila wao kujua.

Katika Makala hii nmekuchambulia baadhi ya vyanzo vikuu vya kupata Minyoo,Soma hapa...

Hivi ndiyo vyanzo vikuu vya minyoo kwa mtu:

1. Kula Chakula kichafu

Kula mboga au matunda yasiyooshwa vizuri

Kula chakula kilichochafuliwa na mayai ya minyoo

Kula nyama au samaki wasioiva vizuri n.k

Vitu hivi huweza kuwa vyanzo vikuu vya wewe kuwa na Shida ya Minyoo

Ushauri: Hakikisha Mazingira ya kuandalia vyakula ikiwemo vyakula vyenyewe vinakuwa Safi

2. Kunywa Maji machafu

Kunywa maji yasiyochemshwa au yasiyotibiwa

Kutumia maji yaliyochafuliwa kupikia au kuosha vyombo

Ushauri: Kunywa maji Safi na Salama,maji yaliyochemshwa,kutibiwa n.k. Pamoja na vyombo vya kuhifadhia maji ya kunywa Viwe Visafi Sana.

3. Usafi binafsi duni

Kutokunawa mikono kabla ya kula au baada ya kutoka chooni huongeza hatari ya kuingiza minyoo kwenye mwili wako

Kucha ndefu zinazohifadhi uchafu na mayai ya minyoo, hii pia ni hatari kwa Watu wengi wanaofuga kucha bila wao kujua.

Ushauri: Hakikisha unanawa mikono kabla ya kula,baada ya kutoka chooni,Usafi wa kucha pia usisahau..

4. Kutembea peku au bila Viatu

Minyoo aina ya hookworm huingia mwilini kupitia ngozi ya mguu

Hutokea zaidi kwenye udongo wenye uchafu wa kinyesi

Ushauri: Usipende kutembea Peku,Vaa Viatu, hata kama ni Mkulima upo shambani usitembee peku kwenye Udongo hii ni hatari zaidi kushambuliwa na minyoo.

5. Vyoo visivyo salama

Kutumia vyoo vibovu au Vichafu sana hii huweza kuongeza hatari ya wewe kupata minyoo

Uchafu wa Vyoo huweza kuhusisha;

  • Mazingira yake kwa ujumla
  • Vyombo vya maji
  • Maji yenyewe yanayotumika n.k.
Pia kujisaidia eneo la wazi huweza kuongeza hatari ya minyoo kwani Huchafua udongo na maji pia.

Ushauri: Hakikisha vyoo vinakuwa Safi na Salama kwa matumizi muda wote

6. Kula Udongo

Wapo baadhi ya Watu hupenda kula Udongo ikiwemo watoto wadogo na wakina mama wajawazito, hii huweza kuwa chanzo kikubwa cha kupata Minyoo pia.

Ushauri: Acha Tabia ya kula Udongo,Lakini pia Mzuie mtoto wako kula Udongo

7. Kuambukizwa kutoka kwa mtu mwingine

Kugusana na mtu mwenye minyoo (hasa watoto)

Kushiriki vyombo, taulo au vitanda bila usafi

Vyote hivi huweza kuongeza hatari ya kupata Minyoo

Je,Una tatizo hilo na hujapata Msaada wa Tiba bado?

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

➡️Dalili za Minyoo Soma hapa:https://www.afyaclass.com/2021/07/dalili-za-minyoo-jamii-ya-ascariasis.html

Rejea Sources:

  • https://www.cdc.gov/dpdx/hookworm/index.html
  • https://emedicine.medscape.com/article/218805-overview
  • https://australian.museum/learn/species-identification/ask-an-expert/what-are-worms/#:~:text=Many%20very%20different%20and%20unrelated,Flatworms%20are%20soft%2C%20unsegmented%20invertebrates.
  • https://www.who.int/news-room/fact-sheets/detail/soil-transmitted-helminth-infections

Consultation ya Afya Moja kwa Moja

Mimi ni Dr. Ombeni Mkumbwa. Nakupa ushauri wa kitaalamu kuhusu tatizo lolote la kiafya kwa siri, haraka na uhakika.

WhatsApp

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code