Kaka wa Michael Jackson afariki Dunia kwa mstuko wa moyo.
Kaka wa marehemu Michael Jackson, aitwaye Tito Jackson, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 70.
Tito pia alikuwa mwanamuziki katika kundi la familia la The Jackson 5, ambalo Michael Jackson alianza kulitumikia tangu akiwa na miaka sita.
Taarifa za kifo chake zimetolewa na Siggy Jackson, ambaye ni mpwa wake kupitia jarida la 'PEOPLE', zikieleza kuwa Tito Jackson amefariki dunia siku ya jana Septemba 15 kwa mstuko wa moyo.
Kupitia kundi la The Jackson 5, Tito alipata umaarufu katika miaka ya 1970 kutokana na nyimbo kama "I Want You Back," "ABC," na "I'll Be Therena."
Hata hivyo, katika kundi hilo alikuwa na uwezo wa kupiga gitaa na kuandika nyimbo ambazo zilisaidia kukuza kundi hilo.
Tito baadaye alijitosa kufanya kazi za peke yake na kufanikiwa kuwa na albamu kama "Tito" (1978) na "I’m a Winner" (1979).
Mbali na kazi za muziki, Tito alikuwa akijihusisha na shughuli za jamii, kama vile kupigania haki za watu na msaada kwa vijana.