Kunyonyesha Mtoto na VVU: Je, mama mwenye VVU anaweza kunyonyesha?

 Kunyonyesha Mtoto na VVU: Je, mama mwenye VVU anaweza kunyonyesha?

Mama mwenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(VVU) kunyonyesha Mtoto.

Yapo baadhi ya Maswali mengi kuhusu unyonyeshaji kwa mama mwenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(VVU), JE ANARUHUSIWA KUNYONYESHA?

Huu hapa ni muongozo Kamili wa Shirika la Afya Duniani(WHO) Kuhusu unyonyeshaji kwa Mama mwenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(VVU);

Muongozo huu ulianza kwa kujibu Swali hili; Je,Mama mwenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(VVU) anaweza kunyonyesha Watoto wake sawa sawa au kama Mama ambaye hana HIV?

Can mothers living with HIV breastfeed their children in the same way as mothers without HIV?

MAJIBU: Muongozo kamili unaanzia hapa,

WHO inapendekeza wakina mama Wote wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(VVU) lazima wapate dawa wakati wote yaani "life-long antiretroviral therapy (ART)" kwa ajili ya kusaidia kuboresha afya zao pamoja na afya za watoto wao.

Muongozo wa Shirika la afya Duniani(WHO) wa Mwaka 2016 July unashauri;

Kwa Nchi Zote ambazo zimeamua kuhamasisha na kusaidia Unyonyeshaji pamoja na Matumizi ya dawa(ART), Wakina mama wote ambao huishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi(VVU) ambao wanatumia dawa kama inavyotakiwa wanapaswa kunyonyesha Watoto Maziwa ya mama pekee kwa kipindi cha Miezi 6 ya Mwanzo.

WHO: "mothers living with HIV who are on ART and adherent to therapy should breastfeed exclusively for the first 6 months",

Miezi Sita(6) hii ya mwanzo,mtoto hunyonyeshwa Maziwa ya Mama Peke yake pasipo kuchanganyiwa na vitu vingine vyovyote,

Kisha baada ya Miezi 6 ya mwanzo, anza kumchanganyia mtoto na vitu vingine vya kula, ila hakikisha unaendelea kumnyonyesha maziwa yako kwa kipindi cha Miaka 2 au Zaidi ukiweza.

"and then add complementary feeding until 12 months of age. Breastfeeding with complementary feeding may continue until 24 months of age or beyond".

KUMBUKA: Unyonyeshaji huu ni kwa Mama mwenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(VVU) ambaye anafuata Mashariti yote ya dawa, Mama anayetumia dawa za ARVs kama inavyopaswa/kwa usahihi.

Mwazoni, WHO ilishauri Mama mwenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(VVU) kunyonyesha kwa miezi 12 tu kisha kuacha kama mama huyu alikuwa anapata mlo kamili na Salama wakati wa unyonyeshaji wake,

Lakini Muongozo mpya ambao umejikita kwenye uthibitisho wa kisayansi unaonyesha kwamba;

Matumizi ya dawa(ART) kwa usahihi husaidia kuzuia maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(VVU) wakati wa Unyonyeshaji kwa kiwango kikubwa,

Muongozo huu mpya unaonyesha kwamba,kuna faida nyingi ambazo mama mwenye maambukizi ya Virusi vya ukimwi anayenyonyesha pamoja na mtoto anayenyonya wanaweza kupata wakati wa unyonyeshaji sawa sawa na mama ambaye hana maambukizi yoyote.

Hivo basi,Shirika la Afya Duniani(WHO) linapendekeza msisitizo uwekwe zaidi kwenye kuboresha mifumo ya utoaji wa huduma za afya ili kutoa huduma bora zaidi kwa Watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(VVU),

Huduma bora ni pamoja na kwenye Swala nzima la utoaji wa dawa za ARVs(ART) Kwa usahihi pamoja na kuendelea kuwahudumia wakina mama wote wanaoishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi(VVU). 



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!