Ticker

6/recent/ticker-posts

Tatizo La Kuvimba Taya,Chanzo,Dalili Na Tiba



 TATIZO LA KUVIMBA TAYA,CHANZO,DALILI NA TIBA

Baada ya kupata Cases nyingi kwenye shida hii, leo nmeamua kukupa ABC kuhusu tatizo hili la kuvimba taya,

je tatizo hili husababishwa na nini?dalili zake pamoja na Tiba yake,

CHANZO CHA TATIZO LA KUVIMBA TAYA

Miongoni mwa sababu za mtu kuvimba taya ni pamoja na;

1. Tatizo la kuvimba kwa tonses(Tonsillitis), hizi ni soft tissues ambazo zipo nyuma ya koo, na kazi yake kubwa ni kuzuia vimelea vya magonjwa kama vile bacteria n.k kuingia ndani ya mwili wako kwa njia ya mdomo au Pua.

Sasa soft tissues hizi zinapovimba(Tonsillitis) husababisha shingo kuvimba na maeneo mengine kama vile kuvimba taya n.k

DALILI AMBAZO MTU HUWEZA KUPATA NI PAMOJA NA;

- kupata shida ya kumeza kitu

- Sauti kutoka inakwaruza,sauti kukauka au mtu kushindwa kuongea

- Mtu kuanza kukohoa

- Kupata maumivu makali ya kichwa,masikio n.k

- Joto la mwili kupanda au mtu kuwa na homa

- Kuhisi kichefuchefu mara kwa mara

- Uchovu wa mwili kupita kiasi n.k

MATIBABU;

• Asilimia kubwa ya dalili hizi za kuvimba tonses(Tonsillitis), huisha,zenyewe ndani ya siku 3 mpaka 4 inachotakiwa kufanya ni;

- Pata muda wa kutosha wakupumzika

- Kunywa maji mengi angalau lita 2.5 mpaka 3 kwa siku

- Tumia dawa za maumivu kama vile paracetum au acetaminophen, ibuprofen n.k

- Na tiba rasimi kama vile matumizi ya dawa jamii ya antibiotics huweza kuanza kama dalili bado zipo hata baada ya siku 4.

2. Maambukizi kwenye koo pamoja na tonses ambayo kwa kitaalam hujulikana kama Strep throat,

Maambukizi haya huhusisha mashambulizi ya group la vimelea vya magonjwa wanaojulikana kama Streptococcusbacteria.

ambapo matokeo yake huweza kuwa,mtu kuvimba tezi za shingoni pamoja na kwenye taya(Neck and jaw Lymph nodes swelling)

DALILI ZAKE NI PAMOJA NA;

- kupata shida ya sore throat

- Kupata maumivu makali wakati wa kumeza kitu

- Kuvimba kwa tonses

- Homa kali

- Kichefuchefu pamoja na kutapika

- Mwili kuchoka kupita kiasi n.k

MATIBABU;

baadhi ya watu wanaweza wasionyeshe dalili zozote lakini wakifanyiwa vipimo vinaonyesha positive strep throat,

na baada ya kupata majibu haya,mgonjwa huweza kuanzishiwa tiba mbali mbali kama vile matumizi ya dawa jamii ya penicillin au amoxicillin n.k

3. Tatizo la kuwa na jipu au Peritonsillar abscess, Mtu huweza kuwa na jipu kwenye eneo la Tonses pamoja na kwenye kuta za koo hali ambayo huweza kupelekea kuvimba kwa Taya lote.

Na miongoni mwa bacteria ambao husababisha tatizo hili ni pamoja na hawa Streptococcusbacteria.

DALILI ZAKE NI PAMOJA NA;

- Kuvimba kwa uso pamoja na taya

- Joto la mwili kuwa juu au mtu kuwa na homa

- Kuvimba kwa tezi za shingoni(swollen neck lymph nodes)

- Sauti kubadilika kabsa(muffled voice)

- Kupata shida wakati wa kumeza kitu

- Kupata shida wakati wa kufungua mdomo

- Kupata maumivu ya kichwa

- Mwili kutetemeka n.k

MATIBABU

Mgonjwa atapata matibabu mbali mbali kama vile matumizi ya dawa za kumeza(oral antibiotics) au kama tatizo ni Serious sana huweza kupata IV antibiotics n.k

4. Maambukizi ya Virusi(Viral infections) kama vile;Measles, mumps, na rubella (MMR), hawa ni miongoni mwa virusi ambao husabababisha sana kuvimba kwa tezi za shingoni(lymph nodes) pamoja na taya(jaw).

pia Mononucleosis  ni maambukizi mengine ya virusi ambao huweza kusababisha kuvimba kwa tezi za shingoni pamoja na Taya.

DALILI ZAKE KWA UJUMLA NI PAMOJA NA;

- Mtu kupata homa

- Mwili kuanza kuwa na rashes

- Kuanza kukohoa

- Kupata shida ya Runny nose

- Macho kuanza kubadilika rangi na kuwa mekundu

- Maumivu makali kwenye misuli,joints na viungo

- Kuvimba kwa tezi za mate(swollen salivary glands)

- Kuvimba kwa taya, Tezi za shingoni

- Kupata maumivu makali ya kichwa

- Hamu ya chakula kupotea kabsa

- Mwili kuchoka kupita kawaida n.k

MATIBABU;

• Njia zuri ni kujikinga kwa kupata chanjo ya MMR vaccination,

Kunywa maji ya kutosha, pata muda mzuri wa kupumzika, tumia dawa za maumivu N.K

5. Tatizo la Lyme disease,ambapo huhusisha maambukizi ya Bacteria wanaojulikana kama Borrelia bacteria,

DALILI ZAKE NI PAMOJA NA;

- Maumivu,kukakamaa na Kuvimba kwa Taya

- Kupata maumivu makali kwenye joints za Taya

- Kuzuia jaw movement

- Kusikika kwa sauti kwenye Taya ambazo ni popping sounds wakati wa kufungua au kufunga mdomo

- Kupata maumivu ya kichwa

- Kupata maumivu ya joints,misuli pamoja na viungo vya mwili

- Mtu kupata shida ya Shingo kukakamaa(neck stiffness)

- Upande mmoja wa uso kushuka chini kidogo

- Kupata kizunguzungu,kukosa pumzi,mapigo ya moyo kwenda mbio n.k

MATIBABU;

Tiba kubwa ya tatizo hili ni matumizi ya dawa jamii ya Antibiotics(Antibiotics are the first line of treatment).

6. Kupata uvimbe kwenye taya(Jaw cysts),
Uvimbe huu huweza kuanzia popote mfano kwenye mfupa wa taya(jawbone) au kuzunguka kwenye root ya Jino.

Na mara nyingi uvimbe huu hutokana na; Jino kuharibika(decaying tooth), jino kuvunjika(broken tooth), Jino kuingia ndani ya mfupa wa taya n.k

DALILI ZAKE NI PAMOJA NA;

- Kuhisi kuchoma choma au ganzi kwenye Lips za mdomo,fizi,au kwenye meno

- Kuwa na nafasi kwenye meno ya karibu ambapo uvimbe umetokea

- Mfupa wa Taya kukosa nguvu

- Taya kuvimba n.k

MATIBABU;

• Kuondoa jino liloharibika,kuvunjika au kuingia ndani ya mfupa wa taya na kusababisha uvimbe,

kufanyiwa upasuaji na kuondolewa Uvimbe huu, pamoja na matibabu mengine kama vile ya dawa jamii ya antibiotics n.k

7. Tatizo la Thyroid nodules pamoja na Thyroid cancer, vyote hivi huweza kupelekea kuvimba kwa Taya.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.