Ugonjwa wa Ebola husababishwa na nini,Dalili na Tiba
Fahamu kuhusu Dalili za Ugonjwa Wa Ebola,chanzo cha ugonjwa wa ebola,pamoja na matibabu ya ugonjwa wa ebola kupitia Makala hii.
Ugonjwa wa Ebola ni miongoni mwa magonjwa hatari ambayo yanaweza kusababisha idadi kubwa ya Vifo,
Kama ilovyoripotiwa kwenye vyombo mbali mbali vya Habari,Ugonjwa wa ebola umewahi kukumba maeneo mbali mbali ikiwemo nchini Uganda,Congo n.k
Dalili za Ugonjwa Wa Ebola
Dalili za Ugonjwa wa ebola huweza kujitokeza kuanzia Siku 2 mpaka siku 21 baada ya mtu kuambukizwa,
Na dalili za Mwanzoni kabsa za ugonjwa wa ebola ni pamoja na;
• Mgonjwa kupata homa
• kupata maumivu ya Viungo,Misuli, maumivu ya kichwa n.k
• Mwili kukosa nguvu na kuwa dhaifu Sana
• Mwili kuchoka sana
• Kukosa hamu ya kula
• Kupata maumivu ya tumbo
• Kuharisha
• Kutapika
• Pamoja na kuvuja damu kwenye maeneo mbali mbali.
Dalili za Ugonjwa Wa Ebola
Kwa Ujumla Dalili za Ugonjwa wa Ebola ni pamoja na;
- Mgonjwa kupata homa kali pamoja na mwili kuchoka sana
- Maumivu makali ya kichwa
- Maumivu kwenye joint,misuli pamoja na viungo mbalimbali vya mwili
- Ngozi ya mwili kuwasha
- Kusikia kichefu chefu pamoja na kutapika
- Kupatwa na tatizo la kuharisha
- Kutokwa na Damu sehemu zote zenye matundu mwilini,kama kwenye masikio,pua na macho.
- Hamu ya chakula kupotea
- Kupata shida wakati wa upumuaji
- Kupata maumivu makali ya kifua
- Kubadilika rangi ya macho na kuwa Nyekundu
- Kupatwa na Homa kali, degedege
- Kutapika matapishi yenye damu
- Kuharisha na kutoa damu machoni
- Kutokwa na damu katika matundu ya mwilini kama vile; Puani,Njia ya haja kubwa,njia ya haja ndogo,mdomoni,masikioni,machoni n.k Hali ambayo hupelekea kifo cha Muda mfupi
UGONJWA WA EBOLA
Ugonjwa wa Ebola ni ugonjwa unaosababishwa na Virusi ambao hujulikana kama Ebola virus,
Virusi hawa wapo wa aina mbali mbali kama vile Ebola-Sudan Strain n.k
HISTORIA YA EBOLA
Kwa mara ya kwanza Ugonjwa wa Ebola ulihusishwa kutokea huko ZAIRE(CONGO) mwaka 1976. Ambapo aina tano za Virusi vinavyosababisha Ugonjwa wa Ebola vilikuja kugundulika hapo baadae,baada ya maeneo mengi kuathiriwa na Ugonjwa huu.
NJIA AMBAZO UGONJWA WA EBOLA HUAMBUKIZWA
Ugonjwa wa ebola huweza kusambazwa kwa njia mbali mbali kama vile;
- Kupitia kugusana na mgonjwa wa Ebola
- Kupitia kwenye Vidonda vilivyopo wazi(open wound)
- Kupitia kugusana na mgonjwa au mnyama aliyekufa mwenye Virusi hawa wa Ebola
- Kupitia kushika au kugusa matapishi ya mgonjwa wa Ebola
- Kupitia maji maji ya mwili wa Mgonjwa,mate,jasho au Damu yake
- Kupitia kugusa au kushika kinyesi au Mkojo wa mgonjwa wa Ebola
- Lakini pia Mtu huweza kupata Ugonjwa wa Ebola kwa Kupitia Wanyama pia
- Kushiriki tendo la Ndoa na Mgonjwa wa Ebola
- Kushirikiana Vyombo vya Kula pamoja na chakula na Mgonjwa wa Ebola
- Kushika mashuka au nguo za mgonjwa wa Ebola bila kuvaa kinga kama Gloves mikononi n.k
Vipimo Vya Ugonjwa wa Ebola
Mgonjwa wa Ebola hufanyiwa vipimo maalum ambavyo huhusisha sampuli za Damu,Mate,jasho N.k kutoka kwa Mgonjwa, Japo mara nyingi vipimo hivo hufanyika baada ya mtu kuhisi ugonjwa huu au kuonyesha baadhi ya Dalili za Ugonjwa huu wa Ebola.
MATIBABU YA UGONJWA WA EBOLA.
Mpaka sasa hakuna matibabu au Dawa ya moja kwa moja kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa Ebola. Bali watu hutibu dalili za Ugonjwa kama ilivyo kwa magonjwa mengi yanayosababishwa na Virusi kama CORONA.
FAQs: Maswali ambayo huulizwa Mara kwa mara
Je,Dalili za Ugonjwa Wa Ebola ni Zipi?
Kwa Ujumla Dalili za Ugonjwa wa Ebola ni pamoja na;
- Mgonjwa kupata homa kali pamoja na mwili kuchoka sana
- Maumivu makali ya kichwa
- Maumivu kwenye joint,misuli pamoja na viungo mbalimbali vya mwili
- Ngozi ya mwili kuwasha
- Kusikia kichefu chefu pamoja na kutapika
- Kupatwa na tatizo la kuharisha
- Kutokwa na Damu sehemu zote zenye matundu mwilini,kama kwenye masikio,pua na macho.
- Hamu ya chakula kupotea
- Kupata shida wakati wa upumuaji
- Kupata maumivu makali ya kifua
- Kubadilika rangi ya macho na kuwa Nyekundu
- Kupatwa na Homa kali, degedege
- Kutapika matapishi yenye damu
- Kuharisha na kutoa damu machoni
- Kutokwa na damu katika matundu ya mwilini kama vile; Puani,Njia ya haja kubwa,njia ya haja ndogo,mdomoni,masikioni,machoni n.k Hali ambayo hupelekea kifo cha Muda mfupi
Hitimisho
Ugonjwa wa ebola ni Miongoni mwa magonjwa hatari ambayo huweza Kusababisha Idadi kubwa ya Vifo ndani ya Muda Mfupi,
Kuna umuhimu mkubwa sana wakufahamu kuhusu dalili za Ugonjwa wa ebola, hii itakusaidia kupata msaada wa haraka ikiwa una dalili hizo pamoja na kujikinga na watu wenye dalili za ugonjwa wa ebola,
Dalili za Ugonjwa wa ebola ni pamoja na;Mgonjwa kupata homa kali pamoja na mwili kuchoka sana,Maumivu makali ya kichwa,Maumivu kwenye joint,misuli pamoja na viungo mbalimbali vya mwili,Ngozi ya mwili kuwasha,
Kusikia kichefu chefu pamoja na kutapika,Kupatwa na tatizo la kuharisha,Kutokwa na Damu sehemu zote zenye matundu mwilini,kama kwenye masikio,pua na macho.
Hamu ya chakula kupotea,Kupata shida wakati wa upumuaji,Kupata maumivu makali ya kifua,Kubadilika rangi ya macho na kuwa Nyekundu,Kupatwa na Homa kali, degedege,Kutapika matapishi yenye damu,Kuharisha na kutoa damu machoni,
Kutokwa na damu katika matundu ya mwilini kama vile; Puani,Njia ya haja kubwa,njia ya haja ndogo,mdomoni,masikioni,machoni n.k Hali ambayo hupelekea kifo cha Muda mfupi,
Ukiona Dalili kama hizi hakikisha unawahi hospital kwa ajili ya Vipimo Zaidi.
0 Comments