Ugonjwa wa Lymphedema,Chanzo na Tiba
Lymphedema ni tatizo ambalo huhusisha kuvimba kunakotokana na Lymph kujikusanya kwenye Tishu mbali mbali za mwili hasa eneo la Mikononi na Miguuni.
Lymph ni maji maji(Fluid) ambayo yana seli nyeupe za damu(white blood cells-WBCs) ambazo hupambana dhidi ya Viini mbali mbali vya magonjwa,
Hivo kwa ujumla huu ni mfumo muhimu wa Kinga ya mwili ambao husaidia kwenye ulinzi dhidi ya magonjwa mbali mbali.
Sasa endapo maji haya(Lymph) yakajikusanya sehemu moja ya tisu za mwili ndipo husababisha kuvimba, na tatizo hili kwa kitaalam hujulikana kama Lymphedema.
Kwa baadhi ya Watu,Tatizo la Lymphedema huanza wiki 6 mpaka 8 baada ya Upasuaji au Tiba ya Mionzi kwa wagonjwa wa Saratani,
Pia huweza kuanza taratibu baada ya Matibabu ya Saratani kuisha, Unaweza kuanza kuona dalili za tatizo la Lymphedema kwa miezi 18 mpaka 24 baada ya Matibabu na wakati mwingine huweza kuchukua hata miaka kuanza.
Zingatia mambo haya Muhimu kama Ugonjwa wa Lymphedema umeathiri mikono na Miguu;
✓ Endapo Ugonjwa wa Lymphedema umesababisha kuvimba Mikono, unashauriwa kutumia mikono yako kufanya kazi zako za kila siku, kama vile kupika,kula,kuvaa,kuoga,kuchana nywele n.k,
✓ Wakati wa kupumzika,weka mikono hii kwenye usawa wa juu kidogo ya Moyo, mara mbili au tatu kwa siku wakati ukiwa umelala.
✓ Hakikisha unalala kwa dakika 45 si chini ya hapo
✓ Pia unaweza kuweka mikono yako juu ya mtu ili iwe huu kidogo wakati umelala
✓ Kunja na kukunjua mikono yako mara 15 mpaka 25 wakati ukiwa umelala.
✓ Hakikisha unatunza ngozi ya mikono na Miguu yenye ugonjwa wa Lymphedema ili isipate michubuko n.k
✓ Kila siku, hakikisha unasafisha mikono na Miguu yako ambayo ina tatizo la Lymphedema, na tumia mafuta kama Lotion ili kuiweka ngozi yako ya Mikono kuwa na unyevu unyevu.
✓ Baada ya kusafisha miguu, hakikisha inakuwa mikavu na vaa soksi zenye material ya Pamba(Cotton soks)
✓ Pia unashauriwa kuvaa Vitu kama gloves mikononi wakati unafanya kazi kama za Bustani n.k
✓ Jikinge pia na Miale mikali ya Jua
✓ Epuka kushika a kukanyaga vitu vya baridi sana au Moto sana
✓ Epuka kuvaa nguo za kubana sana mikono au Miguu ambayo ina tatizo la Lymphedema
✓ Hakikisha unakata kucha zako vizuri, na kama kuna dalili zozote za maambukizi kwenye kucha hakikisha unapata msaada wa kimatibabu
✓ Usitembee hapo chini bila viatu(miguu peku)
✓ Hakikisha miguu imefunikwa vizuri wakati unatembea nje
✓ Epuka kukaa Sehemu moja kwa Zaidi ya dakika 30
✓ Usikunje Miguu yako(maarufu kama kukunja nne) wakati wa Kukaa.
✓ Kwa Wanawake pia wenye tatizo la Lymphedema, wanashauriwa kuvaa Bra ambazo hazibani sana
✓ kama unabeba Kitu kama handbag, tumia Mkono ambao haujaathiriwa na tatizo hili la Lymphedema.
✓ Kama una vidonda au michubuko, nawa taratibu sana kwa maji safi na Sabuni.
✓ Tumia Dawa,mafuta au Cream za kuua viini vya magonjwa eneo la kidonda.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!
Emoji