Ticker

6/recent/ticker-posts

Madhara ya caffeine kwa mjamzito,Epuka vitu vyenye Caffeine



Madhara ya caffeine kwa mjamzito,Epuka vitu vyenye Caffeine

Bila shaka hii sio ngeni kwako,kusikia kuhusu Madhara ya caffeine kwa mjamzito na Ushauri wa wataalam mbali mbali wakishauri kupunguza matumizi ya vitu vyenye caffeine nyingi hasa wakati wa Ujauzito,

Kumbuka:Vinywaji vyenye Caffeine(caffeinated beverages) ni pamoja na;

  • Kahawa
  • Chai
  • Soda
  • pamoja na energy drinks

ila baadhi ya tafiti zinaonyesha hata matumizi ya kiwango cha wastani cha caffeine bado huweza kusababisha madhara kwa ujauzito wako,

Katika makala hii tutachambua Zaidi kuhusu Madhara ya caffeine kwa mjamzito pamoja na Tafiti mbali mbali ambazo zimethibitisha hili.

Madhara ya caffeine kwa mjamzito

Haya hapa ni baadhi ya Madhara ya caffeine kwa mjamzito;

- Kuathiri ukuaji wa mtoto tumboni,

Tafiti zinaonyesha, hata matumizi ya wastani ya Caffeine kila siku bado huweza kusababisha Madhara kwa mjamzito ikiwemo; kuathiri ukuaji wa mtoto tumboni.

Tafiti:Wanawake wajawazito ambao walitumia caffeine ambayo ni sawa na nusu kikombe cha kahawa kwa siku kwa wastani walizaa watoto wadogo zaidi kuliko wajawazito ambao hawakutumia vinywaji vyenye kafeini, kulingana na utafiti katika Taasisi za Kitaifa za Afya.

Mbali na kuathiri ukuaji wa mtoto na Kusababisha kuzaa mtoto mdogo zaidi(smaller birth size) kama Madhara ya caffeine kwa mjamzito, Pia matumizi ya caffeine huweza kuongeza hatari ya watoto kupata matatizo mengine kama vile;

  • Tatizo la unene au obesity,
  • Kupata Magonjwa ya Moyo(heart disease)
  • Pamoja na ugonjwa wa kisukari hapo baadae

- Kuzaa mtoto mwenye tatizo la Uzito mdogo(low birth weight)

Moja ya Madhara ya caffeine kwa mjamzito ni kuongeza hatari ya Kuzaa mtoto mwenye tatizo la Uzito mdogo,

Hii ni kutokana na Caffeine kuathiri kwa kiwango kikubwa Ukuaji wa mtoto akiwa tumboni yaani kwa kitaalam intrauterine growth restriction.

- Kusababisha mishipa ya damu kwenye kizazi(uterus) pamoja na kondo la nyuma(placenta) kubana

Watafiti waligundua pia,Moja ya Madhara ya caffeine kwa mjamzito ni kusababisha mishipa ya damu kwenye kizazi(uterus) pamoja na kondo la nyuma(placenta) kubana/constrict,

Hali ambayo hupelekea kiwango cha damu kinachokwenda kwa mtoto kupungua zaidi kisha kuzuia ukuaji zaidi wa mtoto.

- Pia matumizi ya Caffeine huweza kuvuruga baadhi ya vichocheo kwa mtoto yaani fetal stress hormones,

Na kuongeza hatari Zaidi ya watoto kuwa na matatizo kama vile;

  • Uzito kuongezeka kwa kasi sana mara tu baada ya kuzaliwa
  • Na hapo baadae kuwa na tatizo la obesity
  • magonjwa ya moyo(heart disease)
  • Pamoja na Ugonjwa wa kisukari

Hayo ndyo baadhi ya Madhara ya caffeine kwa mjamzito.

FAQs: Maswali ambayo huulizwa mara kwa mara

Je, matumizi ya Vinywaji vyenye Caffeine ni salama kwa mjamzito?

Kutokana na tafiti mbali mbali,matumizi ya Caffeine au vitu vyenye caffeine sio Salama wakati wa ujauzito, hata kama umetumia kwa kiwango cha wastani.

Hitimisho

Kulingana na tafiti mbali mbali juu ya matumizi ya vitu vyenye Caffeine wakati wa Ujauzito,

Matokeo yanaonyesha Madhara ya caffeine kwa mjamzito ni mengi,

Hii haijalishi umetumia kwa kiwango kikubwa au kiwango cha wastani yaani moderate caffeine consumption,

Madhara ya caffeine kwa mjamzito ni pamoja na kuathiri ukuaji wa mtoto tumboni,kisha kupelekea kuzaa mtoto mdogo,mtoto mwenye uzito mdogo pamoja na matatizo mengine ya kiafya hapo baadae.

Baada ya kufahamu baadhi ya Madhara ya caffeine kwa mjamzito, ni matumaini yangu kwamba utaepuka matumizi ya Vitu vyenye Caffeine katika kipindi cha Ujauzito wako.