Dalili kuu za tatizo la Mzio au Allergy dhidi ya Vitu mbali mbali

Dalili kuu za tatizo la Mzio au Allergy dhidi ya Vitu mbali mbali

#1

Dalili kuu za tatizo la Mzio au Allergy dhidi ya Vitu mbali mbali



Tatizo la mzio (au allergy kwa Kiingereza) ni hali ambayo mfumo wa kinga ya mwili hutambua kitu kisicho na madhara kama tishio, na kujaribu kupambana nacho. Kitu hiki huitwa allergen — kwa mfano: vumbi, poleni, baadhi ya vyakula, dawa, vitu vyenye kemikali flani, baadhi ya Sabuni,Mafuta au manyoya ya wanyama.n.k.

Hizi hapa ni baadhi ya dalili ambazo huweza kukuonyesha kwamba una shida ya Mzio au allergies kwenye baadhi ya Vitu.

1. Kuvimba Pua muda mfupi baada ya kutoka nje, hii ni allergic rhinitis, ambapo mtu hupata reaction dhidi ya particles ndogo kwenye hewa anayovuta.

Kuvimba pua baada ya kukaa sehemu zenye vumbi,kula chakula flani,dawa n.k

2. Mtu kupiga chafya sana hata baada ya kula kitu chochote,

3. Kuwashwa Sana Mwilini, na wakati mwingine kupata vipele kwenye ngozi

4.macho kutoa machozi yenyewe, na baadhi ya watu hupata shida hii baada ya kuanza kunywa dawa ambazo hawajawahi kuzitumia kabsa.

5. Mtu kuvimba Mdomo baada ya kula baadhi ya vyakula

6. Mtu kuwashwa sana masikio au Mdomo, hasa baada ya kula chakula flani

7. Mtu kuvimba mdomo,uso,pua n.k baada ya kuoga kwa kutumia baadhi ya sabuni

8. Kupata shida ya kupumua,kila unapokula nyama au chakula flani



9.Ngozi kubadilika rangi,kuwasha,kuwa na vipele,baada ya kula baadhi ya vyakula,dawa n.k

10. Kupata kichefuchefu,kutapika,maumivu ya tumbo au Kuharisha,kila unavyokula baadhi ya vyakula

11. Mtu kuvimba Ulimi au Lips za mdomo baada ya kula baadhi ya vyakula,Dawa n.k

Dalili zingine za mzio au Allergy zinaweza kujumuisha:

  • Kikohozi, mafua/kujaa kamasi puani
  • Kuwashwa kwa macho, pua au ngozi
  • Kuvimba kwenye uso, midomo, au ulimi
  • Mapigo ya moyo kwenda haraka
  • Ngozi kupata upele au ukurutu (eczema)
  • Kuharisha, kutapika au maumivu ya tumbo (hasa kwa allergy ya chakula)
  • Kuharisha
  • kupumua kwa shida (kwa allergy mbaya sana)
  • Katika hali mbaya sana, mtu anaweza kupata mshtuko mkubwa wa mzio (anaphylaxis) ambapo huhitaji msaada wa haraka sana.

Mzio waweza kutokana na vitu kama vile:

  • Vumbi au ukungu
  • Chakula fulani kama maziwa, mayai, karanga, dagaa,nyama nk.
  • Dawa fulani kama penicillin
  • Sumu ya wadudu kama nyuki
  • Harufu kali au kemikali n.k.

Tiba na ushauri:

  • Epuka kitu kinachosababisha mzio
  • Tumia dawa jamii za antihistamine kwa tatizo hili
  • Wasiliana na daktari kwa vipimo zaidi kama skin prick test au blood test n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Reply


image quote pre code