Magonjwa 15 hatari ambayo ngozi yako inaweza kukupa tahadhari mapema

Magonjwa 15 hatari ambayo ngozi yako inaweza kukupa tahadhari mapema

#1

Magonjwa 15 hatari ambayo ngozi yako inaweza kukupa tahadhari mapema




1. Saratani ya ngozi (Skin cancer)

Ngozi inaweza kuonyesha uvimbe mdogo, vidonda visivyopona, madoa meusi yanayopanuka au kubadilika rangi, au mabadiliko ya alama za kuzaliwa (moles). Saratani ya ngozi kama melanoma ni hatari sana ikiwa haitagunduliwa mapema.

2. Saratani ya ini (Liver cancer)

Ngozi ya mtu mwenye shida kubwa ya ini inaweza kuanza kuwa ya njano (jaundice), ikimaanisha ini halifanyi kazi vizuri. Saratani ya ini au uvimbe mkubwa unaweza kuathiri kazi za ini mapema.

3. Homa ya ini (Hepatitis B na C)

Magonjwa haya huathiri ini, na dalili za ngozi zinaweza kujitokeza kama manjano ya macho na ngozi, kuwasha mwili mzima, na maumivu ya juu kulia mwa tumbo. Kuchelewa kupata matibabu kunaweza kupelekea Madhara Zaidi

4. Kisukari (Diabetes)

Ngozi inaweza kuonyesha dalili kama vidonda visivyopona, ngozi kuwa nyeusi na nene hasa shingoni au kwapani (acanthosis nigricans), kuwashwa sana, na maambukizi ya mara kwa mara ya fangasi au bakteria.

5. Shinikizo la damu la juu (Hypertension)

Ingawa halionekani moja kwa moja kwenye ngozi, shinikizo la damu la muda mrefu linaweza kuathiri mzunguko wa damu, kuleta uvimbe wa miguu, na mara nyingine mishipa midogo ya ngozi huathirika, ikionekana kama mishipa iliyopasuka.



6. UKIMWI (HIV/AIDS)

Huu ugonjwa unaweza kuanza kuonyesha dalili za ngozi mapema, kama vipele vya rangi nyekundu au zambarau, vidonda mdomoni, mdomo kupata vidonda ambavyo haviishi.

7. Lupus

Lupus ni ugonjwa wa kinga mwili unaposhambulia mwili wako. Ngozi inaweza kuonyesha vipele vya butterfly shape usoni, uwekundu unaozidi kwenye jua, na mabadiliko ya kucha.

8. Upungufu wa damu (Anemia)

Ngozi ya mgonjwa wa anemia huwa ya rangi ya kufifia (pale), midomo(lips) na mdomo wa ndani pia hupoteza rangi, na wakati mwingine ngozi huonekana kavu zaidi.

9. Ugonjwa wa figo (Kidney disease)

Ngozi inaweza kuwa kavu sana, ya kupauka, na kuanza kuwasha sana. Wakati figo hazitoi sumu vizuri nje ya mwili, dalili hizi hujitokeza. Miguu na uso pia vinaweza kuvimba.

10. Ugonjwa wa moyo (Heart disease)

Ngozi ya vidole, midomo au kucha inaweza kugeuka ya bluu (cyanosis) ikiwa moyo haupeleki oksijeni vizuri. Vilevile, miguu na mikono inaweza kuvimba kutokana na msongamano wa maji.

11. Ugonjwa wa tezi (Thyroid disease)

Tatizo la Hypothyroidism hufanya ngozi kuwa kavu, baridi na nywele kunyonyoka.Wakati Hyperthyroidism huleta hali ya joto kali, ngozi kubadilika na viganja vinavyotokwa jasho sana.

12. Ugonjwa wa Homa ya uti wa mgongo (Meningitis)

Ngozi inaweza kuonyesha vipele vidogo vya rangi ya zambarau au nyekundu ambavyo havipotei ukivibinya, mara nyingi pamoja na homa kali na shingo kuwa ngumu.

13. Shida za mapafu (Lung disease)

Ngozi ya vidole au midomo inaweza kuonyesha rangi ya bluu kutokana na upungufu wa oksijeni. Vidole vinaweza kuwa na ncha pana (clubbing).n.k.

14. Ugonjwa wa mishipa ya damu (Peripheral vascular disease)

Ngozi ya miguu inaweza kuwa baridi, kupoteza nywele, kuwa nyembamba na kupata vidonda visivyopona kutokana na mzunguko mbaya wa damu.

15. Ugonjwa wa Saratani ya damu (Leukemia)

Ngozi inaweza kuonyesha madoa ya rangi nyekundu (petechiae), michubuko isiyoelezeka, na mara nyingine wekundu kwenye ngozi kutokana na upungufu wa platelet au kuvuja damu chini ya ngozi.

Hitimisho:
Ngozi yako siyo tu kifuniko cha mwili, bali ni kioo cha afya ya ndani. Ukiona dalili zisizo za kawaida kama madoa, vidonda, kuwasha sana au kubadilika kwa rangi, ni vyema kumuona daktari mapema.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Reply


image quote pre code