Marekani yapunguza msaada kwa Zambia kutokana na wizi wa dawa na vifaa tiba

Marekani yapunguza msaada kwa Zambia kutokana na wizi wa dawa na vifaa tiba

#1

Marekani yapunguza msaada kwa Zambia kutokana na wizi wa dawa na vifaa tiba



Marekani imetangaza kuwa kupunguza msaada wa $50m (£37m) kwa sekta ya afya ya Zambia, kutokana na nchi hiyo kushindwa kushughulikia "wizi wa kimfumo" wa dawa na vifaa tiba vilivyotolewa.

Uamuzi huu "mgumu" ulichukuliwa baada ya onyo la mara kwa mara kwa serikali ya Zambia kulinda dawa muhimu kwa ajili ya wagonjwa walio hatarini zaidi nchini humo, alisema balozi wa Marekani nchini Zambia Michael Gonzales.

"Hatuko tayari tena kukubali kunufaisha walaghai au mafisadi wakati wagonjwa wanakosa au kununua dawa za kuokoa maisha ambazo tumetoa bure," aliongeza.

Serikali ya Zambia ilisema imechukua hatua za kukabiliana na suala hilo.

Waziri wa Afya Elijah Muchima aliishukuru Marekani kwa "msaada wake wa ukarimu",

Hatua hii ya Marekani kwa Zambia ni tofauti na kusitishwa kwa misaada ya kigeni iliyotangazwa na Rais Donald Trump mnamo Januari.

Lakini maafisa wa Marekani walisema wamegundua "wizi wa nchi nzima" wa bidhaa za matibabu ambazo zilikusudiwa kusambazwa bure kwa umma na sasa zinauzwa na maduka ya dawa ya binafsi.

Zaidi ya maduka ya dawa 2,000 kote nchini Zambia yalipatikana yakiuza dawa na vifaa tiba vilivyotolewa katika uchunguzi wa mwaka mzima uliofanywa na ubalozi wa Marekani.

"Kwa hali ya kushangaza, katika ziara hizi, asilimia 95 ya maduka ya dawa yaliyokuwa yakiuza aina ya bidhaa ambazo Marekani hutoa, pia walikuwa wakiuza bidhaa za wizi," ilisema taarifa hiyo.

Takribani nusu ya maduka ya dawa yaliyotembelewa yalipatikana yakiuza dawa na vifaa vilivyotolewa na serikali ya Marekani, ilisema.

Maduka mengine ya dawa pia yalikuwa yakiuza hisa za matibabu zilizoibiwa zilizonunuliwa na serikali ya Zambia, Mfuko wa dunia na wafadhili wengine, iliongeza.

Reply


image quote pre code