Sababu za Kichwa kuwasha,Soma hapa kufahamu
Kuwashwa kwa kichwa (itchy scalp) ni hali inayoweza kusababishwa na sababu mbalimbali. Hizi hapa ni sababu kuu zinazoweza kusababisha hali hii;
1. Tatizo la Fangasi wa kichwani au kwenye ngozi
Hii ni hali ya ngozi inayosababisha uwekundu, magamba, na kuwashwa. zipo fangasi kama vile Malassezia,Tinea capitis n.k.
Ringworm (Tinea Capitis)
Ni maambukizi ya fangasi yanayoathiri kichwa. Husababisha maeneo yenye mviringo au vibarango, nywele kunyonyoka na kuwashwa kichwani.2. Tatizo la Ngozi kuwa Kavu (Dry Scalp)
Ngozi ya kichwa inapokuwa kavu, huweza kuwasha. Hali hii husababishwa na hewa kavu, kuoga kwa maji ya moto, au kutumia shampoos kali.
3. Tatizo la Mzio (Allergic Reaction) au Contact Dermatitis
Baadhi ya bidhaa za nywele zinaweza kusababisha kuwashwa kwa kichwa, kama vile rangi ya nywele au shampoos.
Na Sababu kubwa inakuwa shida ya Mzio au Allergy dhidi ya hivo vitu.
4. Psoriasis ya Kichwa
Huu ni ugonjwa wa ngozi unaosababisha seli kukua haraka sana, na kuunda magamba meupe na ngozi nyekundu. Lakini huweza kusababisha dalili hii ya kuwashwa Kichwani.
5. Tatizo la Pumu ya ngozi au Eczema (Atopic Dermatitis)
Hii Ni hali ya muda mrefu inayosababisha ngozi kuwa kavu, kuwasha pamoja na maumivu. Inaweza kuathiri kichwa.
6. Chawa wa Kichwa (Head Lice)
Hawa Ni wadudu wadogo wanaoishi kwenye nywele na husababisha kuwashwa, hasa nyuma ya masikio na kwenye shingo.
7. Tatizo la Folliculitis
Haya ni maambukizi ya vinyweleo vya nywele yanayosababisha vipele vidogo na kuwashwa.
8. Urticaria (Hives)
Ni vipele vyekundu vinavyotokea ghafla kutokana na mzio. Huambatana na kuwashwa kikali.
Matibabu yake huhusisha dawa jamii ya antihistamines.
9. Sababu Nyingine:
- Scabies (Sarcoptes scabiei): Wadudu wanaochimba chini ya ngozi.
- Acne miliaris necrotica: Viuvimbe vya usaha kwenye kichwa.
- Magonjwa ya autoimmune: K.m. lupus na dermatomyositis.
- Kutokuosha kichwa vizuri
- Uzalishwaji wa mafuta mengi kwenye ngozi ya kichwa n.k.
Vyanzo vya Maelezo:
- Healthline: https://www.healthline.com/health/itchy-scalp
- Medical News Today: https://www.medicalnewstoday.com/articles/itchy-scalp
- Harvard Health: https://www.health.harvard.edu/diseases-and-conditions/what-could-be-causing-your-itchy-scalp
- Cleveland Clinic: https://health.clevelandclinic.org/itchy-scalp-common-problems-and-fixes
- American Academy of Dermatology: https://www.aad.org/public/everyday-care/itchy-skin/itch-relief/relieve-scalp-itch
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
Reply
image quote pre code