Ugonjwa wa Goita,Chanzo,dalili na Tiba

Ugonjwa wa Goita,Chanzo,dalili na Tiba

#1

Ugonjwa wa Goita,Chanzo,dalili na Tiba



Goita (Goiter) ni hali ya kuvimba kwa tezi ya thyroid. Uvimbe huu hautokani na saratani (goita si saratani). Tezi ya thyroid ipo sehemu ya mbele ya shingo. Kazi kuu za tezi ya thyroid ni kuzalisha homoni mbalimbali ambazo husaidia mwili kuthibiti na kufanya kazi zake mbalimbali.

Visababishi vya Goita

  • Upungufu wa iodini kwenye chakula (sababu kuu katika maeneo mengi).
  • Magonjwa ya kinga mwilini kama Hashimoto’s thyroiditis au Graves’ disease.
  • Kuvimba kwa tezi kwa sababu zisizojulikana.
  • Matumizi ya dawa au kemikali fulani.
  • Uzazi na mabadiliko ya homoni, hasa kwa wanawake.

FAHAMU: Sababu kuu ya Goita kwenye maeneo mengi ni kutopata iodine ya kutosha katika lishe. Iodine ni madini muhimu yanayohitajika katika utengenezaji wa homoni mbalimbali zinazozalishwa na tezi ya thyroid. 

Watu wanaoishi kwenye maeneo mbali kutoka pwani ya bahari au yaliyo katika nyanda za juu kutoka usawa wa bahari kama vile mikoa ya Mbeya, Iringa na Rukwa wapo katika hatari ya kupata goita kwa vile hawapati madini ya kutosha ya Iodine katika chakula chao.

•Soma: Ugonjwa wa Mgongo Wazi kwa Watoto,chanzo,Dalili na Tiba yake

Dalili Za Ugonjwa wa GOITA 

Dalili kuu ya goita ni kuvimba au kuongezeka ukubwa kwa tezi ya thyroid. Ukubwa wa tezi unaweza kuwa kijiuvimbe kidogo katika tezi au uvimbe mkubwa kama nundu sehemu ya mbele ya shingo.

Dalili zingine za Goita

  • Kikohozi kisichoisha
  • Kupata shida ya kumeza au kupumua
  • Sauti kubadilika
  • Dalili za hyperthyroidism (kama moyo kwenda mbio, jasho, kupunguza uzito) au hypothyroidism (uchovu, baridi, kuongezeka uzito) n.k.

Kuvimba kwa tezi ya thyroid kunaweza kusababisha mgandamizo katika njia ya hewa na mrija wa chakula, hali ambayo inaweza kusababisha:

1. Shida katika kupumua

2. Kikohozi

3. Sauti kuwa ya mikwaruzo

4. Shida wakati wa kumeza chakula

5. Wakati mwingine, mishipa ya damu ya shingoni inaweza kuvimba pia na kusababisha mtu kujihisi kizunguzungu pindi anapoinua mikono juu n.k

Matibabu ya Ugonjwa wa Goita

  • Matumizi ya iodini(hasa kwenye goita ya kawaida)
  • Dawa za kudhibiti homoni za thyroid
  • Upasuaji kama goita ni kubwa mno au inasababisha matatizo ya kupumua/kumeza n.k.
  • Tiba ya mionzi (Radioactive iodine), hasa kwa goita yenye sumu

Kinga Zaidi kwa Shida hii ya Goita

  • Kula chumvi yenye iodini
  • Lishe bora yenye vyakula kama dagaa, samaki, maziwa, na mayai
  • Kuepuka vyakula vinavyopunguza kazi ya thyroid (kama vile mihogo mibichi, kama inaliwa mara kwa mara bila kupikwa vizuri)

Je,Una tatizo hili na bado hujapata Tiba?

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!




Reply


image quote pre code