Elon Musk hajawahi kupitia umasikini maishani mwake,Baba yake Errol Musk asimulia
Elon Musk hajawahi kupitia umasikini maishani mwake, alienda shuleni kwa Rolls Royce kila siku." ___ Errol Musk, baba yake Elon Musk afichua
"Ninamjua mwanangu, Elon Musk, anajaribu kuwahamasisha watu na wao wawe Matajiri lakini hapaswi kusema uongo ili kufanya hivyo. Elon Musk hakukulia katika Familia ya umasikini kama anavyodai. Kwa kweli, alienda shuleni kwa Rolls Royce kila siku.
Na siyo Rolls Royce Hizi ndogo, bali Rolls Royce Corniche convertible ya kifalme. Nilimsaidia kuanzisha kampuni yake ya kwanza, kwa hivyo ingawa anataka kuwahamasisha wengine kuwa alianza kutoka sifuri, ukweli ni kwamba mtaji ni muhimu sana katika biashara yoyote, na alifanikiwa kwa sababu alikuwa na mtaji ambao nilimsaidia Mimi Baba yake." ~ Errol Musk
Nyuma ya kila hadithi ya motisha, kuna shujaa asiyejulikana, na baba yake Elon Musk ndiye shujaa asiyejulikana katika hadithi yake.
Kwa nini waliofanikiwa huhisi kuwa wanapaswa kusema uongo ili kuwahamasisha wengine
REPLY HAPA
image quote pre code