Hofu kuhusu Unyanyasaji wa Wazee kwenye Vituo vya kulelea wazee
Leo tarehe 15 mwezi Juni ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu unyanyasaji dhidi ya wazee ambapo maudhui ya mwaka huu wa 2025 ni kusaka suluhu ya vitendo hivyo vya unyanyasaji kwenye vituo vinavyotoa huduma ya malezi ya muda mrefu kwa wazee.
Tafiti zinaonyesha licha ya kuongezeka kwa hamasa juu ya uwepo wa vitendo hivyo vya ukatili, bado mataifa mengi hayana takwimu za uhakika na zilizochambuliwa kuhusu vitendo hivyo.
Halikadhalika mataifa hayo katika vituo hivyo hakuna watumishi wa kutosha na hata walioko hawana mafunzo ya kutosha ya kulea wazee, jambo linaloweka mazingira ya vitendo vya ukatili na hata wazee kutelekezwa.
Watoa huduma wakiri kuonea wazee
Utafiti ulioungwa mkono na shirika la Afya duniani WHO ulionesha kuwa takribani asilimia 64 ya watendaji walioko kwenye vituo vya malezi ya wazee walikiri Kutenda vitendo vya ukatili dhidi ya wazee mwaka uliopita.
“Hali hii inaonesha dhahiri udharura wa kuleta mabadiliko ya kimfumo,” unasema Umoja wa Mataifa(UN).
Mambo ya kuzingatia
Kwa mantiki hiyo, maadhimisho ya mwaka huu yatajikita kwenye ukatili wanaokumbana nao wazee katika vituo vinavyotoa huduma za malezi yao kwa muda mrefu.
Umoja wa Mataifa unasema, ijapokuwa wazee wengi wanaishi kwenye jamii zao, huduma za kwenye vituo vya malezi ni uhalisia kwa wengi.
“Wakati huu ambapo mahitaji ya malezi kwenye vituo yakiongezeka kutokana na ongezeko la wazee duniani, vivyo hivyo hofu kuhusu ulinzi wa haki za wazee, usalama wao na utu wao wakiwa kwenye vituo hivyo,” unasema Umoja Mataifa.
REPLY HAPA
image quote pre code