Benki ya NMB  yazindua Programu Maalum ya Ujuzi

Benki ya NMB yazindua Programu Maalum ya Ujuzi

#1

SERIKALI imeipongeza Benki ya NMB  kwa kuzindua Programu Maalum ya Ujuzi kwa Maendeleo ya Ujasiriamali na Ajira kwa Vijana (SEED), inayolenga kuwaongezea vijana wa Kitanzania Maarifa na Ujuzi wa kujiajiri, pamoja na kuwasaidia mitaji ya kuanzisha na kuendeleza biashara zao wenyewe.



SEED inatekelezwa kwa pamoja kati ya NMB Foundation na Save the Children, ambayo kwa kuanzia itawafikia vijana 200 kutoka Vyuo vya Ufundi jijini Dar es Salaam, vya VETA Dar es Salaam, Kipawa ICT Center na Kigamboni Folk Development College, ambao watapatiwa mafunzo mbalimbali.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa programu hiyo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, alisema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, imekuwa na mpango endelevu wa ujenzi wa Vyuo vya Ufundi katika kila wilaya, hivyo inahitaji uungwaji mkono.

Katika uzinduzi huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya NMB Foundation, Bi. Ruth Zaipuna, alisema SEED ni matunda ya maono ya pamoja baina ya benki yake na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, yaliyoangazia namna ya kusaidia vijana kujiendeleza kiuchumi.

“Leo tuko hapa kuonesha namna Ujasiriamali unavyoenda kutekelezwa kwa vitendo na NMB kupitia NMB Foundation, kuwasaidia Watanzania, hususani Vijana 200 tunaoenda kuanza nao ili kuwa sehemu ya suluhisho la Changamoto ya Ajira nchini, ambako watapatiwa Mafunzo na Elimu ya Usimamizi wa Fedha.

Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa NMB, Foundation, Nelson Karumuna, alisema msukumo wa wazo lililozaa SEED ni takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, iliyoonesha kuwa idadi ya vijana Tanzania ni asilimia 34.5, ambako katika vijana 10, wanne kati yao hawana ajira au fursa za kujikwamua kiuchumi.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Save the Children, Angela Kauleni, alisema Tanzania, ambayo kimakadirio ina watu karibu milioni 70, inahitaji nguvu za ziada katika uwekezaji na uwezeshaji vijana katika kutimiza ndoto zao za kukua kiuchumi na kielimu.

Related Discussions

REPLY HAPA


image quote pre code