Daktari Bingwa wa Watoto afariki kwa kujinyonga
Daktari Bingwa wa Watoto wa Hospitali Teule ya Kibosho iliyoko Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro, Dk. Magret Swai, amepoteza maisha, baada ya kudaiwa kujinyonga.
Akithibitisha kutokea kwa tukio leo Julai 14, 2025 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), Simon Maigwa, amesema kuwa daktari huyo, alipoteza maisha Julai 10 mwaka huu, majirani ya saa 3 usiku.
SACP Maigwa amesema tukio hilo limetokea Kata ya Longuo, ambapo mwanamke Magreth Swai (30), alijinyonga kwa kutumia waya wa antena uliokuwa umefungwa kwenye nondo ya mlango wa chumbani kwake.
"Chanzo cha tukio hilo ni msongo wa mawazo uliotokana na afya ya akili ambapo Marehemu alifungua waya huo kwenye nondo iliyopo juu ya mlango na kujitundika" amesema SACP Maigwa.
RPC Maigwa ameongeza kuwa marehemu alianza kuugua ugonjwa wa afya ya akili akiwa katika mafunzo kwa vitendo kama Daktari maalum wa watoto wa miaka minne iliyopita.
REPLY HAPA
image quote pre code