Elon Musk atangaza kuanzisha chama chake kipya cha Kisiasa,America Party

Elon Musk atangaza kuanzisha chama chake kipya cha Kisiasa,America Party

#1

Bilionea na mkurugenzi wa kampuni ya Tesla na X (zamani Twitter), Elon Musk, ametangaza kuanzisha chama kipya cha siasa kinachoitwa America Party  akisema lengo lake ni kurudisha uhuru kwa wananchi wa Marekani ambapo hatua hii ikiwa ni ya kujibu hali ya kisiasa ambayo kwa maoni yake inafanya kazi kama mfumo wa chama kimoja.



Tangazo hilo limekuja baada ya kufanya kura mtandaoni kupitia jukwaa lake la X ambapo zaidi ya Watu milioni moja walipiga kura na asilimia 65 wakaunga mkono kuanzishwa kwa chama hicho na Musk ameeleza kuwa chama hicho hakitalenga kugombea urais bali kitawania viti vichache katika Bunge la Marekani ili kuleta ushawishi wa kweli kwenye mchakato wa kutunga sheria.

Elon Musk pia amedokeza kuwa chama hicho kitaweka mkazo katika kupunguza matumizi ya serikali, kupambana na urasimu na kulinda uhuru wa Raia, ingawa hajaeleza kwa undani sera rasmi za chama hicho kwa sasa ila Watu wengi wameona hatua hii kama muendelezo wa tofauti zake za wazi na Rais wa Marekani, Donald Trump.

Hata hivyo inaonekana chama kipya kitaingia kwenye changamoto kubwa hasa kutokana na mfumo wa Marekani wa vyama viwili vikuu (Democrat na Republican) ambapo ni vigumu kwa chama kipya kupata nafasi ya kujiimarisha kitaifa na hadi sasa haijajulikana ni wanasiasa gani au Watu mashuhuri watakaojiunga naye.

Related Discussions

REPLY HAPA


image quote pre code