Balozi wa Tanzania nchini Cuba na aliyekuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Humphrey Hesron Polepole ametangaza kujiuzulu Ubalozi leo July 13 2025.
Katika barua yake ya wazi kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambayo ameichapisha katika kurasa za mitandao yake ya Kijamii leo Julai 13, 2025 Polepole amesema amefikia hatua hiyo kwa tafakuri ya kina juu ya mwelekeo wa sasa wa uongozi Nchini.
Polepole amesema uamuzi wake umetokana na kushuhudia kwa masikitiko makubwa kudidimia kwa maadili ya uongozi, kutojali haki na maslahi ya Wananchi pamoja na kuporomoka kwa dhamira ya dhati ya kuwatumikia Wananchi katika ngazi mbalimbali za serikali ambapo amesema hali hiyo imemnyima amani ya moyo.
Aidha, Polepole amekosoa vikali mwenendo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika mchakato wa uteuzi wa Wagombea, akisema misingi ya Chama na kauli mbiu ya “Chama kwanza mtu baadaye” imepuuzwa na kwamba baadhi ya Viongozi wameweka mbele maslahi ya Watu au Makundi binafsi kuliko Taasisi ya Chama.
Polepole amemshukuru Rais Samia kwa nafasi na imani aliyompa kuwa mwakilishi wa Taifa akisema historia itatoa tafsiri sahihi ya hatua hiyo aliyoichukua.
REPLY HAPA
image quote pre code