Jenerali Muhoonzi Kainerugaba ambaye ni mtoto wa Rais Museveni ameibua gunzo nchini Uganda baada ya kutangaza nia yake ya kuwa Rais baada ya baba yake.
“Kwa jina la Yesu Kristo Mungu wangu nitakuwa Rais wa nchi hii baada ya baba yangu” aliandika Muhoonzi katika ukurasa wake wa X jana Julai 16,2025.
Ujumbe huo uliibua mjadala kuhusu mustakabali wa uongozi na uwezekano wa kuendelea kwa familia ya Museveni katika Mamlaka.
Hii sio mara ya kwanza kwa Jenerali Muhoonzi kutoa matamko kama hayo japo kauli ya sasa hivi inaonekana kuwa ya kumaanisha zaidi. Tyari baba yake, Rais Museveni ametangaza na kupitishwa na chama chake NRM kuwa mgombea Urais mwakani. Hiyo itakuwa ni mara ya nane kwa Museveni mwenye miaka 82 kugombea urais nchini Uganda.
image quote pre code