Je,Umepaliwa ghafla wakati unakula chakula,Fanya haya haraka

Je,Umepaliwa ghafla wakati unakula chakula,Fanya haya haraka

#1

Ukimeza chakula vibaya na ukapaliwa (choking), zifuatazo ni hatua za haraka za kujiokoa:

Ikiwa UMEPALIA WEWE MWENYEWE:

JARIBU KUKOHOA KWA NGUVU

Kohoa kwa nguvu mara kadhaa ili kujaribu kusukuma chakula kilichokwama kutoka kwenye koo.

JIPIGE MGONGONI

Tumia mkono mmoja jipige mgongoni kwa nguvu.

TUMIA "ABDOMINAL THRUST" (Heimlich Maneuver):

Simama na jiweke mikono katikati ya tumbo, chini ya mbavu.

bana kwa nguvu ndani na juu (kama unataka kutoa kitu).

Rudia mara kadhaa (5 au zaidi) hadi chakula kitoke.

KUMBUKA:

Ukiona mtu hawezi kuongea,kashindwa kabsa kupumua,au kapoteza fahamu, hiyo ni dharura ya haraka.

Chukua hatua mara moja – ya kuwahi hospitalini.

#afyaclass #chakula #kupaliwa #huduma

Consultation ya Afya Moja kwa Moja

Mimi ni Dr. Ombeni Mkumbwa. Nakupa ushauri wa kitaalamu kuhusu tatizo lolote la kiafya kwa siri, haraka na uhakika.

WhatsApp

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code