Maambukizi ya ugonjwa wa Mpox yaongezeka Kenya

Maambukizi ya ugonjwa wa Mpox yaongezeka Kenya

#1

Mamlaka za afya nchini Kenya zimeripoti kuongezeka kwa kasi kwa maambukizi ya ugonjwa wa Mpox katika kaunti ya pwani ya Mombasa, kusini mashariki mwa Kenya



Mombasa ni miongoni mwa majimbo 21 yaliyoathiriwa na mlipuko huo, ambapo maambukizi ya kwanza eneo hilo yalithibitishwa Septemba mwaka jana.

‘’Kuna maambukizi mengi eneo la Mombasa kwa sababu jamii haijakubali kuwa ugonjwa huu upo,’’ Dk Mohamed Hanif, mkurugenzi wa huduma za matibabu wa kaunti, aliwaambia waandishi wa habari siku ya Ijumaa.

Kufikia mwisho wa wiki, tangu mwaka jana, Mombasa ilikuwa imerekodi maambukizi 98 yaliothibitishwa na vifo viwili. Wakaazi wengi wamechanganya vipele vya Mpox kuwa hali nyingine kama vile ugonjwa wa ndui au vipele vya joto.

“Wagonjwa wengi wana umri wa kati ya miaka 24 na 45. Mtoto mdogo zaidi ana umri wa miaka 12. Sote tuko hatarini,” alisema Dk Hanif.

Tangu Kenya kutangaza mlipuko wa Mpox tarehe 31 Julai 2024, Wizara ya Afya imethibitisha maambukizi 226 na vifo vinne nchini kote.

Vituo vya Afrika vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Afrika CDC) vinasema visa vingi vya magonjwa ya MPOX vinashuhudiwa katika nchi zenye kiwango cha juu cha magonjwa kama VVU au kifua kikuu mfano Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Sierra Leone, lakini kwa sasa Mpox inaongezeka nchini Kenya na Guinea huku Uganda na Burundi pia wakishuhudia kuibuka tena kwa ugonjwa huo.

Hivi karibuni Kenya ilirekodi kiwango cha juu cha visa vya ugonjwa huo kwa kila wiki, ikiashiria kuwa huenda awali, visa vingi havikuwa vinatambuliwa, shirika hilo lilisema.

Nchini Kenya, maambukizi ya kwanza ya ugonjwa wa Mpox yalitambuliwa katika ukanda wa usafiri wa kaskazini kati ya madereva wa malori, wanaojihusisha na biashara ya ngono na wafanyabiashara. Sasa maambukizi yanaenea kwenye jamii, ambayo inatoa changamoto mpya", alisema Dk Yap Boum II, naibu mkuu wa timu ya msaada ya usimamizi wa matukio ya CDC ya Afrika, wakati wa kikao cha kila wiki siku ya Alhamisi.

"Tunahitaji kusaidia Kenya na uchunguzi. Dozi 10,000 za chanjo zinapatikana lazima zisambazwe kwa njia mahususi ili kudhibiti mlipuko huo kabla ya kuenea zaidi," ameongeza.

MPOX inasalia kuwa dharura ya afya ya umma ugonjwa uliosababisha wasiwasi kimataifa.

Related Discussions

REPLY HAPA


image quote pre code