Maandamano kenya Leo,takribani watu 11 wamefariki na wengine kujeruhiwa

Maandamano kenya Leo,takribani watu 11 wamefariki na wengine kujeruhiwa

#1

Dakika chache baada ya saa nane mchana wa Alhamisi Juni 25, 2024 hali tete iliyokuwa inatokota nje ya majengo ya Bunge la Kenya, iliharibika kabisa na kuwa mbaya.



Umati mkubwa wa vijana ambao ulikuwa unakabiliana na polisi wa kuzima ghasia asubuhi hiyo, uliwashinda nguvu maafisa wa usalama na kuvunja ua wa Bunge na hatimaye kuingia ndani.

Ni katika wakati huu ambapo historia ilikuwa inaandikwa na kunakiliwa kwenye vitabu vya kumbukumbu nchini humo. Alipolala muanzilishi wa taifa Mzee Jommo Kenyatta - aliyeshirikiana na MAUMAU kupigania haki za Wakenya – ndipo ambapo vijana walipitia wakielekea ndani ya majengo ya bunge wakitaka kuwashinikiza wabunge kutupilia mbali mswada wa fedha wa 2024 ambo walikuwa wameupitisha.

Risasi zilirindima angani kwa muda ambao kwa waliokuwa wanafuatilia kwenye runinga – ulionekana kama mwaka mzima – na kelele ilipotulia, kilio kilifuata, huku maiti ya vijana kadhaa ikilala nje ya Bunge hilo kwenye barabara ya parliament hapa Nairobi.

Mpaka Sasa takribani watu 11 wamefariki na wengine kujeruhiwa.

Related Discussions

REPLY HAPA


image quote pre code