Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama, jana Julai 16 alijitokeza kwa mshangao katika kipindi cha podcast ya 'IMO with Michelle Obama and Craig Robinson,' kujibu fununu za yeye kuachana na mkewe.
“Ni vizuri sana kuwaona nyote wawili kwenye chumba kimoja,” alisema Robinson, ambaye ni kaka yake Michelle Obama. Michelle akajibu, “Najua, kwa sababu tusipoonekana pamoja, watu hudhani tumeachana.”
Michelle Obama amekanusha uvumi wa talaka kwa kusema, "Hakujawahi kuwa na wakati wowote katika ndoa yetu ambapo nilifikiria kumuacha mume wangu. Tumepitia nyakati ngumu sana, lakini pia tumekuwa na nyakati nyingi za furaha, na safari nyingi za kipekee. Nimekuwa mtu bora zaidi kwa sababu ya mwanaume niliyeolewa naye.”
Kwa upande Rais Mstaafu, Barack Obama alishangaa, "Fununu hizi ni mojawapo ya mambo ninayoyakosa, hata sifahamu kama suala hili bado linazungumziwa. Nikiulizwa nashangaa!"
Uvumi kwamba wameachana ulianza mapema mwaka huu baada ya mke wa rais wa zamani kutoonekana katika matukio kadhaa makubwa ikiwemo kuapishwa kwa Donald Trump na mazishi ya Rais wa zamani Jimmy Carter.
Wawili hawa walifunga ndoa mwaka 1992 na wana watoto wawili Natasha (anafahamika zaidi kama Sasha) na Malia.
image quote pre code