Polepole ajiuzulu Ubalozi, Amos Makalla atoa neno

Polepole ajiuzulu Ubalozi, Amos Makalla atoa neno

#1

Humphrey Polepole, amejiuzulu Ubalozi wa Cuba.



Kwa mujibu wa barua iliyosambaza jana kwenye mitandao yake ya kijamii, aliandika kuwa amefikia uamuzi huo baada ya tafakari ya muda mrefu.

"Uamuzi huu si mwepesi, bali umetokana na tafakari ya kina juu ya mwenendo wa uongozi katika nchi yetu, uzoefu wangu kama Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Novemba 2020 Machi 2022), na hatimaye kama Balozi,"amesema.

Amesema kwa muda mrefu amekuwa akitafakari kauli ya CCM isemayo "Chama kwanza mtu baadaye", mwanzoni mwa mwaka huu, nilipoona kauli hii inafanyika vinginevyo, nimejiuliza mara kadhaa ni maslahi ya nani yanapiganiwa wakati huu, mtu, kikundi au chama taasisi?

"Kwa kuwa siwezi kuendelea kuwa sehemu ya uongozi usiohamasika na utii wa misingi ya katiba ya nchi na chama, haki, maadili, utu na uwajibikaji kwa wananchi, nimeamua kwa hiari yangu kujiuzulu nafasi yangu ya uongozi na utendaji serikalini."

"Nitaendelea kuwa mwana CCM wa kawaida, mzalendo na raia mwaminifu kwa Taifa na nchi yetu."

Aidha, amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini.



Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla.

Naye, Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla amesema ameiona barua ya Balozi Polepole mtandaoni na kwamba yeye mwenyewe ndio mwenye kuthibitisha uhalali wake.

Makalla ameyasema hayo leo jijini Dodoma baada ya kuulizwa kuhusu barua inayosambaa mtandaoni ya Polepole.

Amesema endapo atathibitisha kama ni ya kwake maudhui ni ya kwake ni utashi wake lakini ambalo limemfurahisha ni kwamba amemalizia kwa kusema atabaki kuwa mwanachama muadilifu wa CCM.

Related Discussions

REPLY HAPA


image quote pre code