Ripoti ya awali ya Ajali ya ndege ya Air India iliyopata ajali mwezi mmoja uliopita mjini Ahmedabad imebaini kuwa swichi za mafuta kwenye moja ya injini za ndege hiyo zilihamishwa kutoka RUN na kwenda CUTOFF sekude chache kabla ya ndege hiyo kuruka.
Ripoti hiyo imebainisha kwamba Katika mazungumzo yaliyonaswa na wachunguzi kwenye rekoda ya sauti ya marubani mmoja alimuuliza rubani mwenzake kwa mshangao “Kwa nini umezikata?” lakini mwenzake alikana kufanya hivyo ambapo jambo hilo linaashiria kwamba usambazaji wa mafuta kwenye injini ulisimamishwa ghafla na kusababisha kushindwa kwa injini zote mbili.
Baada ya swichi kuzimwa, rekodi zinaonesha marubani walijaribu kuzirejesha tena kwenye hali ya “RUN” ili kuokoa hali lakini tayari ndege ilikuwa katika hatari na mfumo wa FADEC, unaosimamia kuwashwa tena kwa injini kiotomatiki ulianza kazi lakini ndege ilishindwa kupata nguvu za kutosha kuruka. Rekodi ya data ya ndege ilikatika muda mfupi baadaye na mara moja rubani alituma ishara ya dharura ya “MAYDAY” lakini hakujibu tena mawasiliano kutoka kwa waelekezi wa trafiki ya anga. Ripoti hiyo imeeleza.
Ndege hiyo ilianguka sekunde 32 tu baada ya kuruka nje kidogo ya uwanja wa ndege na kuangukia hosteli ya wanafunzi wa udaktari ambako ililipuka ambapo zaidi ya watu 270 walipoteza maisha wakiwemo abiria 241 kati ya 242 waliokuwa kwenye ndege na takribani watu 30 waliokuwa ardhini na ndege ilikuwa imejaa mafuta wakati wa ajali, jambo lililochangia mlipuko mkubwa.
Rubani mkuu Kapteni Sumeet Sabharwal alikuwa mkufunzi mwenye uzoefu wa saa 8,200 za urushaji na msaidizi wake Clive Kundar alikuwa na saa 1,100 ambapo Ripoti imethibitisha kuwa wote wawili walikuwa katika hali nzuri kiafya na walikuwa wamestarehe vya kutosha kabla ya safari. Hakuna ushahidi wa awali ulioashiria hujuma, lakini uchunguzi umeangazia onyo la zamani la Mamlaka ya Ndege ya Marekani (FAA) kuhusu uwezekano wa swichi za mafuta kuwa na hitilafu ya kufungwa vizuri.
REPLY HAPA
image quote pre code