Tanzania yazindua kampeni ya Chanjo ya Mifugo na Utambuzi

Tanzania yazindua kampeni ya Chanjo ya Mifugo na Utambuzi

#1

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeanza utekelezaji wa kampeni ya kitaifa ya Chanjo na Utambuzi wa Mifugo Wilayani Longido ambapo takribani mifugo 2000 imechanjwa.



Tukio hilo lililoongozwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji Julai 02, 2025 limefanyika ikiwa ni takribani wiki mbili baada ya Uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu.

Akizungumza wakati wa utekelezaji wa kampeni hiyo Mhe. Dkt. Kijaji amewataka wafugaji wote nchini kutumia fursa hiyo iliyotolewa na Rais Samia kupitia ruzuku ya nusu bei kwa upande wa Ng’ombe, Mbuzi na Kondoo na chanjo ya bila gharama yoyote kwa upande wa kuku wa kienyeji.

“Naomba wataalam wote wa Mifugo tusikae ofisini twendeni uwandani tukatatue changamoto zote za wafugaji” Ameongeza Mhe.Dkt. Kijaji.

Aidha Dkt. Kijaji ameongeza kuwa Serikali imeamua kuendesha kampeni hiyo ili kuiwezesha nchi kuuza mifugo na mazao yake kwenye masoko ya nje ambayo awali yalishindwa kupokea kutokana na changamoto ya kutokuwa na ithibati ya Usalama wa Mifugo na Mazao yake ambapo amebainisha kuwa tayari nchi za Misri na Falme za kiarabu zipo tayari kuanza kununua mifugo hai kutokana na jitihada hizo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Kenan Kihongosi amemhakikishia Dkt. Kijaji kuwa wafugaji wa mkoa huo wapo tayari kuchanja mifugo yao na kutambua kupitia hereni za kielektroniki huku pia akiwataka wafugaji kuendelea kufuga kisasa ili kuinua uchumi wa mkoa huo ambao idadi kubwa ya wananchi wake ni Wafugaji.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji Wilayani Longido Bw. Joseph Sadera ameishukuru Serikali kwa kuwapatia ruzuku kwenye chanjo hizo ambapo ameongeza kuwa jambo hilo limewaongezea chachu ya kufuga kisasa na kuboresha maisha yao kupitia masoko ya mifugo na mazao yake watakayopata baada ya kuchanja mifugo yao.

Mhe. Dkt. Kijaji anatarajiwa kuendelea kukagua utekelezaji wa zoezi hilo katika mikoa ya Mara, Simiyu,Tabora, Geita, Pwani, Morogoro na Dodoma.

Related Discussions

REPLY HAPA


image quote pre code