Tatizo La Sauti Kukauka,Chanzo Na Tiba Yake

Tatizo La Sauti Kukauka,Chanzo Na Tiba Yake

#1

Tatizo la sauti kukauka ni hali ambayo mtu anapoteza sauti au sauti inakuwa ngumu kutoka (hoarseness). Mara nyingi huambatana na maumivu au hali ya kuhisi koo kavu.



Visababishi vya Sauti Kukauka:

  1. Maambukizi ya virusi au bakteria:
    • Mafua, homa ya kawaida, au homa ya mafua (flu).
    • Maambukizi ya koo (pharyngitis) au koo kuvimba.
  2. Kutumia sauti kupita kiasi:
    • Kusema sana, kupiga kelele, au kuimba kwa muda mrefu.
  3. Kukohoa sana:
    • Kukohoa mara kwa mara kunachosha mishipa ya sauti.
  4. Alerji (Aleji):
    • Hasa zinazohusiana na vumbi, poleni, au harufu kali.
  5. Uvutaji sigara au moshi:
    • Moshi huathiri koo na mishipa ya sauti.
  6. Kukauka kwa koo (dehydration):
    • Kutokunywa maji ya kutosha au mazingira yenye hewa kavu.
  7. Tatizo la Acid Reflux (GERD):
    • Asidi kutoka tumboni inapopanda hadi koo, huunguza koo na mishipa ya sauti.
  8. Matatizo ya mishipa ya sauti (vocal cord nodules, polyps, paralysis):
    • Huathiri vibaya utoaji wa sauti.
  9. Msongo wa mawazo au Hofu:
    • Hali ya kiakili inaweza kukausha sauti kwa baadhi ya watu.
  10. Matumizi ya dawa fulani:
  • Dawa za pumu, antihistamine, au dawa za presha.

Dalili Zinazoweza Kuambatana:

  • Koo kukauka.
  • Maumivu ya koo.
  • Sauti kuwa nzito au kubadilika.
  • Kukohoa.
  • Kupiga chafya.
  • Kukohoa damu (mara chache kwenye magonjwa makubwa).
  • Homa au mwili kulegea (kama ni maambukizi).

Ushauri:

  1. Pumzisha sauti:
    • Epuka kuzungumza sana au kupiga kelele.
  2. Kunywa maji mengi:
    • Angalau lita 2 kwa siku kusaidia koo kurainika.
  3. Epuka vinywaji vyenye caffeine, pombe na sigara
  4. Pata Msaada kutoka kwa Wataalam wa afya kama tatizo linaendelea.

1. Hali ya baridi, Wakati unaongea hewa hupita kwenye Voice Box ndani ya Koo lako kisha hugonga kwenye sehemu inaitwa VOCAL CORDS,

Na sauti ya mtu husikika endapo kumetokea hali ya Vibration, Sasa basi,hewa ya baridi sana ikipenya ndani huweza kusababisha shida mbali mbali kama vile kuvimba kwa Vocal Cords hali ambayo huathiri vibration na sauti kutoka nje.

TIBA YAKE: Punguza kuongea sana na kunywa vitu vya kimiminika zaidi kama maji n.k

2. Kutumia sauti sana, hapa tunazungumzia matumizi ya sauti kupita kiasi,mfano kama vile kuongea sana au kuimba sana, hii huweza kusababisha tatizo la sauti kukauka.

TIBA YAKE: Punguza kuongea sana au kuimba sana,kisha pumzisha sauti yako

3. Uvutaji wa Sigara, Watu wengi hawajui kwamba sigara zina madhara mengi yakiwemo; kuathiri utendaji kazi wa Vocal Cords, hali ambayo husababisha matatizo ya kudumu kwenye Sauti yako,

Baadhi ya tafiti zinaonyesha kwamba Wanaovuta sigara wanauwezekano wa kupatwa na matatizo kwenye sauti zao mara 3 zaidi ya ambao hawavuti sigara,

Pia uvutaji wa sigara huongeza hatari ya mtu kupatwa na tatizo la uvimbe yaani Polyp ambao huweza kutokea eneo la vocal cords

4. Tatizo la Allergies au Mzio, Shida ya Allergy huweza kusababisha eneo la Vocal cords kuvimba na kusababisha matatizo ya sauti kama vile sauti ya mtu kukauka n.k

- Mtu kukohoa sana, hii huweza kuvuta misuli eneo la koo pamoja na Vocal cords hali ambayo huweza kusababisha pia tatizo la sauti kukauka,

- Matumizi ya dawa jamii ya Antihistamines kwa ajili ya kutibu allergies, huweza pia kukausha kabsa unyevu unyevu au Mucus kwenye koo lako

5. Tatizo la Rheumatoid arthritis,Shida hii huweza kusababisha matatizo kama vile maumivu,kuvimba kwa joints, n.k

Ila tafiti zinaonyesha kwamba, Kwenye Watu watatu(3) wenye ugonjwa wa Rheumatoid arthritis mmoja(1) wao lazima awe na matatizo kwenye sauti yake

6. Matatizo kwenye tezi la Thyroid,ikiwa ni pamoja na Tezi la thyroid kushindwa kutengeneza kiwango cha kutosha cha vichocheo au hormones

7. Shida ya Gastrointestinal reflux disease(GERD) ambapo husababisha acid ya tumboni kupanda juu kwenye njia ya chakula au Esophagus, hali hii huweza kusababisha matatizo mbali mbali kama vile kiungulia(heartburn) lakini pia shida kwenye sauti ya mtu

8. Shida ya Acute Laryngitis,ambapo sauti ya mtu hupotea kwa gafla

9. Matatizo kwenye mfumo wa fahamu kama vile ugonjwa wa Parkinson, ambao huweza kuathiri misuli ya kwenye uso na kooni,

Karibu asilimia 90% ya Wagonjwa wa Parkinson hupatwa pia na matatizo kwenye sauti zao,ikiwa ni pamoja na maongezi au speech

10. Shida ya Laryngeal cancer,Saratani hii huweza kusababisha matatizo mbali mbali kama vile,maumivu wakati wa kumeza kitu,maumivu ya masikio,mtu kushindwa kupumua,lakini pia hata matatizo kwenye sauti yake.

11. Matatizo mengine ambayo huathiri eneo la vocal cords,kama vile kuwepo kwa Nodules, Polyps, Cysts N.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Related Discussions

REPLY HAPA


image quote pre code