Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi kwa nafasi mbalimbali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jioni hii Julai 16 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, viongozi walioteuliwa ni Omari Juma Mkangama kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Ludewa, Juma Abdallah Njeru kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Mpanda na Bi. Hellen Emmanuel Mwambeta kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha.
Wengine ni Francis Genes Kafuku ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Dkt. Adam Omar Karia ameteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo cha Maji kwa kipindi cha pili, Balozi Dkt. Aziz Ponary Mlima ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi (TISEZA),
Rais pia amemteua Jenerali Mstaafu Venance Salvatory Mabeyo ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro kwa kipindi cha pili, Dkt. Harrison George Mwakyembe ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kwa kipindi cha pili.
Aidha, Filbert Michael Mponzi ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Sukari Tanzania kwa kipindi cha pili na Dkt. Leonada Raphael Mwagike ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA) kwa kipindi cha pili.
REPLY HAPA
image quote pre code