Ugonjwa wa Lupus,chanzo,dalili Zake

Ugonjwa wa Lupus,chanzo,dalili Zake

#1

Ugonjwa wa Lupus ni ugonjwa sugu wa kinga ya mwili (autoimmune disease) ambapo mfumo wa kinga wa mwili hushambulia tishu na viungo vyake badala ya kulinda mwili dhidi ya vijidudu. Lupus inaweza kuathiri ngozi, viungo au (joints), figo, ubongo, moyo, mapafu, na sehemu nyingine za mwili.



AINA ZA LUPUS

Kuna aina kuu nne za lupus:

  1. Systemic Lupus Erythematosus (SLE) – Hii ndiyo aina inayotokea sana na kali zaidi. Inaweza kuathiri viungo vya ndani ya mwili kama moyo, figo, mapafu, na ubongo.
  2. Cutaneous Lupus – Huathiri ngozi. Dalili zake huonekana kama vipele au upele wa mviringo unaoacha kovu.
  3. Drug-Induced Lupus – Husababishwa na baadhi ya dawa. Dalili huisha baada ya kuacha kutumia dawa hiyo.
  4. Neonatal Lupus – Aina adimu inayotokea kwa watoto wachanga wanaozaliwa na mama mwenye lupus.

CHANZO CHA LUPUS

Chanzo kamili cha lupus hakijulikani, lakini kuna mambo kadhaa yanayochangia kupata ugonjwa huu:

  • Urithi (genetics): Historia ya kifamilia ya lupus huongeza uwezekano.
  • Mazingira (environmental triggers): Kama vile mwanga mkali wa jua (UV rays), virusi, maambukizi, na sumu fulani.
  • Homoni: Lupus huwapata zaidi wanawake, hasa wa umri wa uzazi (miaka 15–45), na homoni ya estrogeni inaaminika kuwa na mchango.
  • Dawa: Baadhi ya dawa (kama hydralazine, procainamide) zinaweza kusababisha lupus ya muda.

DALILI ZA LUPUS

Dalili za lupus hutofautiana mtu kwa mtu, lakini za kawaida ni:

  • Uchovu kupita kiasi na wa muda mrefu(chronic fatigue)
  • Homa ya mara kwa mara
  • Maumivu ya viungo (joint pain) na uvimbe
  • Kuwa na Upele usoni (butterfly rash) – unaoanzia mashavuni hadi puani
  • Nywele kupungua/kupukutika
  • Maumivu ya kifua (hasa wakati wa kupumua)
  • Vidonda mdomoni au puani
  • Mikono na miguu kuwa baridi au kubadilika rangi (Raynaud’s phenomenon)
  • Kutoona vizuri au matatizo ya macho
  • Kupungua uzito bila sababu
  • Msongo wa mawazo, matatizo ya kumbukumbu, au kifafa (ikiwa ubongo umeathiriwa)

DALILI ZA UGONJWA WA LUPUS NI ZIPI?

Ugonjwa wa Lupus huweza kuonyesha dalili halafu baada ya mda dalili zikapotea kabsa, alafu zikarudi tena hapo baadae.

 Miongoni mwa dalili hizo ni pamoja na;

1. Mgonjwa kupata vipele maeneo mbali mbali ya mwili kama vile usoni

2. Kuwa na tatizo la kupungua uzito wako wa mwili kwa kasi sana

3. Mwili kuchoka kupita kiasi na kukosa nguvu

4. Joto la mwili kupanda/kuwa juu au Mgonjwa kupata homa

5. Mgonjwa wa Lupus huweza kupata maumivu ya misuli,joint pamoja na viungo mbali mbali vya mwili

6. Mgonjwa kupatwa na hali kama ya mwili kutetemeka au kutingishwa

7. Kuwa tatizo la kukosa hamu ya kula chakula

8. Mgonjwa kuwa na tatizo la kuishiwa na damu

9. Ngozi kubadilika rangi katika maeneo mbali mbali ya mwili na kuwa nyekundu Mfano; kwenye Mikono

MADHARA YA LUPUS

Ikiwa haitatibiwa vizuri, lupus inaweza kusababisha madhara makubwa, yakiwemo:

  1. Magonjwa ya figo (Lupus nephritis): Moja ya madhara makubwa zaidi, na inaweza kuhitaji usafishaji damu (dialysis) au kupandikizwa figo.
  2. Shambulio la moyo na kiharusi: Lupus huongeza hatari ya kupata maradhi haya.
  3. Matatizo ya mapafu: Kama pleuritis (uvimbe wa utando wa mapafu).
  4. Madhara kwa ubongo na mfumo wa neva: Kizunguzungu, kifafa, matatizo ya kumbukumbu.
  5. Upungufu wa damu (anemia) na matatizo ya chembechembe za damu.
  6. Kuathiri mimba: Huweza kusababisha kuharibika kwa mimba au kujifungua mapema.
  7. Maambukizi ya mara kwa mara: Kinga ya mwili ya lupus huwa dhaifu kutokana na ugonjwa wenyewe au dawa zinazotumika.

MATIBABU YA LUPUS

MATIBABU YA UGONJWA HUU WA LUPUS

- Hakuna tiba ya moja kwa moja kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa Lupus,bali kuna tiba ya kudhibiti dalili zinazosababishwa na ugonjwa wa Lupus, 

Mfano; Kama Mgonjwa ataonyesha dalili za mwili kutetemeka atapewa dawa za kuzuia hali hyo, kama anapata maumivu sana,atapewa dawa za kuzuia hali ya maumivu N.K,

 lakini moja ya tiba muhimu huhusisha mgonjwa kupewa dawa ya kupunguza kinga ya mwili kama kinga ya mwili ipo juu sana.

WATU WALIOPO KWENYE HATARI YA KUPATA UGONJWA WA LUPUS

- Ni pamoja na wanawake, kwani zaidi ya asilimia 80% Wanaopata tatizo hili ni Wanawake

- Watu wenye kinga kubwa ya mwili

- Watu wanaotumia dawa zinazohusiana na kupandisha kwa kiasi kikubwa kinga ya mwili

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

USHAURI WA KUISHI NA LUPUS

  • Epuka jua kali – vaa nguo za kujikinga na jua.
  • Pata usingizi wa kutosha na punguza msongo wa mawazo.
  • Fuata lishe bora – Kula kwa wingi mboga za majani, matunda, na vyakula vingine vyenye protini ya kutosha.
  • Fanya mazoezi mepesi mara kwa mara.
  • Wasiliana mara kwa mara na daktari kwa ufuatiliaji wa afya.
  • Epuka kuvuta sigara na pombe.

Ukihisi una dalili zinazofanana na lupus, ni vyema kumwona daktari kwa uchunguzi zaidi (Unaweza kufanya vipimo vya damu: ANA, ESR, dsDNA n.k.).

Related Discussions

REPLY HAPA


image quote pre code