Ripoti ya UNIRANKS ya mwaka 2025, imeangazia vyuo vikuu bora kutoka nchi mbalimbali duniani kwa kuzingatia mambo kadhaa muhimu yanayoonesha ubora wa chuo.
Miongoni mwa vigezo vilivyotumika ni pamoja na ubora wa elimu inayotolewa, mafanikio katika tafiti za kitaaluma, namna chuo kinavyojitangaza, ushirikiano wake na vyuo vingine vya kimataifa, pamoja na mchango wake katika jamii inayokizunguka.
Kwa upande wa Tanzania, jumla ya vyuo vikuu 31 vimethibitishwa na kuingia kwenye orodha rasmi ya mwaka huu.
Hivi ni vyuo vikuu 10 bora zaidi nchini Tanzania mwaka 2025;
1. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)
2. Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA)
3. Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbil (MUHAS)
4. Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)
5. Chuo Kikuu Ardhi (ARU)
6. Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afya na Sayansi Shirikishi (CUHAS)
7. Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira (TUMA)
8. Chuo Kikuu Cha Taifa Zanzibar (SUZA)
9. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT)
10. Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU)
Chanzo: UNIRANKS
REPLY HAPA
image quote pre code