Waziri ajiuzulu baada ya kauli tata kuhusu ombaomba

Waziri ajiuzulu baada ya kauli tata kuhusu ombaomba

#1

Waziri wa Kazi wa Cuba, Marta Elena Feitó Cabrera.



Waziri wa Kazi wa Cuba, Marta Elena Feitó Cabrera, amejiuzulu baada ya kukosolewa vikali kufuatia kauli yake iliyodai kuwa hakuna ombaomba nchini humo.

Akizungumza katika kikao cha Bunge la Kitaifa, Feitó alidai kuwa watu wanaochakura takataka wanatafuta “pesa rahisi,” kauli iliyozua hasira kubwa kwa wananchi, wanaharakati na viongozi, akiwemo Rais Miguel Díaz-Canel.

Kauli hiyo ilionekana kupuuza hali ngumu ya maisha inayowakabili Wacuba wengi, wakiwemo wanaotaabika na umaskini na uhaba wa chakula.Wanaharakati na wasomi walimtaka ajiuzulu wakieleza kuwa matamshi yake ni dharau kwa wananchi.

Kutokana na shinikizo hilo na lawama kutoka ndani na nje ya nchi, Feitó alitangaza kujiuzulu kwake wiki hii.

Chanzo: BBC

Related Discussions

REPLY HAPA


image quote pre code