Abiria wanene kulipia Siti mbili kwenye ndege
Shirika la Ndege la Southwest Airlines Nchini Marekani, limetangaza sera mpya ambayo itawaathiri moja kwa moja Wasafiri wenye miili mikubwa ambao kuanzia Januari 27 2026 watalazimika kulipia siti mbili badala ya moja iwapo miili yao haitoenea vizuri ndani ya siti moja.
Kabla ya sera hii mpya, Shirika hili hapo awali limekuwa likiwaruhusu Abiria waliokosa nafasi ya kutosha kuomba kiti cha ziada bure au kukinunua mapema na kurejeshewa fedha zao baadaye.
Mabadiliko haya yanakuja wakati ambapo Shirika hilo linakabiliwa na changamoto za kifedha na shinikizo kutoka kwa Wawekezaji wa ndani wanaotaka Kampuni hiyo kuongeza faida ambapo mwaka jana Shirika hilo pia lilitangaza kuwa litaanza kutoza ada kwa nafasi za miguu zaidi.
image quote pre code