CCM yaahidi ajira mpya 5,000 sekta ya afya, ajira 7,000 sekta ya elimu.
CHAMA Cha Mapinduzi ( CCM) kimejinasibu kuimarisha sekta ya elimu na afya, ambapo katika miaka mitano ijayo kimeahidi kutoa msukumo serikalini ili kutangazwa ajira mpya 5,000 sekta ya afya, ajira 7,000 sekta ya elimu.
Mgombea Mwenza wa Urais CCM, Dk. Emmanuel Nchimbi alieleza hayo jana wilayani Magu mkoani Mwanza, ikiwa ni mwendelezo wa kampeni za Uchaguzi Mkuu. Dk. Nchimbi alisema endapo CCM ikifanikiwa kushinda katika uchaguzi huo ajira 5,000 mpya zitatangazwa sekta ya afya na ajira 7,000 za walimu wa sayansi na hisabati.
Vilevile, alisema wanafunzi wa shule za msingi watapata mafunzo mazuri kwa lengo la kuwawezesha kujua kusoma, kuandika na kuhesabu.
image quote pre code