Je ni mzigo gani unakulemea? ni Ugonjwa,maumivu moyoni,huzuni,laana,nguvu za giza,Ulevi,kifungo cha kupata hasara,madeni,roho ya kukataliwa,roho ya mauti;unawaza kujiua tu?
Hapana,thamani yako ni kubwa Mno,Mungu anakupenda sana! huna sababu ya kuumia,huna sababu ya kuwa kwenye kifungo hicho,Mkabidhi Yesu maisha yako akuweke huru,Nawe utakuwa huru kweli kweli.
Mkabidhi Yesu Mzigo wako akupe Pumziko,Nawe utapata raha nafsini mwako.
(Soma Mathayo 11:28-29)
"Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu"
image quote pre code