Modeli zote nne za iPhone 17 kuzalishwa nchini India
Kampuni ya teknolojia ya Marekani, Apple, imefanya maamuzi ya kuzalisha modeli zote nne za iPhone 17 nchini India, hatua inayolenga kupunguza gharama kubwa za kodi za uagizaji (tariffs) zilizowekwa na Rais Donald Trump kwa bidhaa zote zinazoingizwa kutoka China.
Uzalishaji huo umegawanywa kati ya makampuni mawili makubwa: Tata Group, lililopo Tamil Nadu, na Foxconn, ambalo lina kiwanda jijini Bangalore.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Apple, Tim Cook, alieleza mapema mwaka huu kuwa kampuni hiyo imeamua kuhamishia uzalishaji wa iPhone 17 nchini India, japokuwa China itaendelea kuwa msambazaji mkuu wa vifaa vinavyotumika katika utengenezaji wa simu hizo.
Hata hivyo, licha ya mabadiliko haya, bei ya iPhone 17 inatarajiwa kupanda kwa kiwango kikubwa itakapowasili sokoni. Apple inategemea kuzindua rasmi iPhone 17 mwezi Septemba mwaka huu, huku tetesi zikidai kwamba simu hiyo itakuja na mwonekano mwembamba zaidi (slim body), rangi mpya, maboresho ya kamera, pamoja na mfumo mpya wa uendeshaji wa iOS 26, ambao unatajwa kuwa uundwaji wa kipekee kwa muongo mzima.
image quote pre code