Mtu aliyejihami kwa bunduki tatu aua wanafunzi wawili kanisani Minneapolis Marekani.
Shirika la upelelezi la Marekani FBI limeanzisha uchunguzi dhidi ya kisa cha mtu aliyekuwa na bunduki kuua watoto wawili kanisani kwa kuwapiga risasi.
Kisa hicho kimetokea jana Jumatano katika kanisa la Kikatoliki huko Minneapolis ikiwa ni wiki ya kwanza ya shule kufunguliwa. Watu wengine 17 walijeruhiwa.
Mshambuliaji ametambuliwa kama Robin Westman mwenye umri wa miaka 23 na alijihami kwa bunduki tatu ikiwemo bastola.
Wapelelezi wanajaribu kubaini ni kwa nini mtu aliyejihami hivyo, awashambulie wanafunzi wanaohudhuria ibada kanisani.
Mkuu wa polisi wa Minneapolisi Brian O'Hara amesema mshambuliaji huyo baadaye alikufa kwa kujiua.
Kisa hicho kinaongeza matukio ya mashambulizi ya bunduki dhidi ya raia nchini Marekani.
image quote pre code