Mwandishi mkongwe wa habari Erick David Nampesya, amefariki dunia

Mwandishi mkongwe wa habari Erick David Nampesya, amefariki dunia

#1

Mwandishi mkongwe wa habari na aliyewahi kuitumikia BBC World Service nchini Tanzania, Erick David Nampesya, amefariki dunia huko Kibamba, Dar es Salaam.



Awali, alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mloganzila jijini humo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa jamaa zake wa karibu, marehemu Nampesya alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Homa ya Ini (Hepatitis), ingawa pia aligundulika kuwa na vidonda vya tumbo.

Nampesya aliyezaliwa mwaka 1969, na aliyekuwa akiripotia Idhaa ya Kiswahili ya BBC, alikumbwa pia na majeraha makubwa kichwani baada ya kuanguka vibaya, anguko ambalo alilielezea mwenyewe takribani miezi miwili kabla ya kifo chake.

Katika maelezo aliyotoa mwezi Mei 2025, Nampesya alisema:

"Nilianguka kwenye sehemu ngumu, nikagonga kichwa na kupata uvujaji wa damu wa ndani."

Hata hivyo, baadaye alithibitisha kuwa hali yake iliimarika baada ya kufanyiwa upasuaji.

Siku mbili kabla ya kifo chake, Nampesya alikuwa akifuatilia kwa karibu mechi ya timu ya Taifa ya Tanzania – Taifa Stars, na hata kuandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kuwa alivutiwa sana na kiwango cha timu hiyo uwanjani.

David alikuwa mwenye ushiriki mkubwa mtandaoni, kiasi cha kwamba aliweza hata kupakia video fupi ya Salim Kikeke, aliyekuwa mtangazaji wa BBC, ambaye kwa sasa alikuwa akigombea ubunge jimbo la Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro, kupitia mchujo wa chama tawala unaoendelea nchini Tanzania.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code