Screen chanzo cha magonjwa ya Moyo kwa Watoto

Screen chanzo cha magonjwa ya Moyo kwa Watoto

#1

Utafiti mpya umebaini kuwa kutumia muda mwingi kwenye vifaa vya kielektroniki kama Simu, Televisheni, Kompyuta na Michezo ya video kunaweza kuathiri si tu afya ya akili ya Watoto na vijana, bali pia afya ya mwili hususan afya ya moyo na mfumo wa Metaboli.



Utafiti huo, uliochapishwa leo katika Jarida la Chama cha Moyo cha Marekani (Journal of the American Heart Association), uliochunguza data kutoka zaidi ya washiriki 1,000 waliokuwa sehemu ya tafiti mbili zilizofanyika Denmark. 

Ripoti hiyo imesema kuwa Watoto wa umri wa miaka 10 na vijana wa miaka 18 waliotumia muda mwingi kwenye vifaa hivyo walionekana kuwa katika hatari kubwa ya kupata magonjwa ya moyo na metaboli kama shinikizo la juu la damu, kolesteroli nyingi na upungufu wa uwezo wa insulini kudhibiti sukari mwilini.

Watafiti walipima hatari ya kila mshiriki kwa kutumia alama maalum kulingana na wastani wa kundi zima, ambapo alama ya 0 ilimaanisha hatari ya wastani na 1 ilimaanisha kiwango cha juu cha hatari kwa kipimo cha standard deviation, ilibainika kuwa kila saa ya ziada ya matumizi ya skrini iliongeza hatari ya ugonjwa kwa asilimia 0.08 kwa watoto wa miaka 10, na asilimia 0.13 kwa vijana wa miaka 18.

Mwandishi Mkuu wa Utafiti huo, David Horner kutoka Chuo Kikuu cha Copenhagen, Denmark amesema kuwa ingawa ongezeko la hatari kwa kila saa ni dogo, linapojumlishwa hadi saa tatu, tano au hata sita kwa siku.

Kwa wastani, vijana wa miaka 18 walikuwa wanatumia takribani saa 6 kwa siku kwenye vifaa hivyo, huku watoto wa miaka 10 wakitumia saa 3 kwa siku, Utafiti pia uligundua kuwa usingizi uliathiri uhusiano huo kulala muda mfupi au kulala kwa kuchelewa kuliongeza hatari ya matatizo ya moyo kwa watoto wanaotumia muda mwingi kwenye skrini. 

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code