Tanzania ni moja kati ya nchi zilizopewa nafasi ya fursa ya masomo katika nchi tano ikiwemo Ghana, Nigeria, Ethiopia, Kenya.
Akizungumza na Mtandao wa HabariLeo mapema hii leo, wakati wa uzinduzi wa ufadhili wa masomo wa Next Gen African Scholarship, Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Veridian Christian (VCU), Dk Tia Murry amesema mpango wa kipekee unaolenga kuongeza upatikanaji wa elimu bora ya mtandaoni yenye msingi wa imani kwa viongozi chipukizi barani Afrika.
“Mpango huu wa ufadhili utawanufaisha watu bora kutoka katika mataifa matano yanayoshiriki ni Tanzania, Ghana, Ethiopia, Nigeria, na Kenya ambao wataonyesha uwezo mkubwa wa uongozi, kujihusisha kwa kina na jamii, na dhamira ya kuleta mabadiliko chanya katika mataifa yao na zaidi.
Amesema fursa hiyo inafaida za Ufadhili wa Masomo kwa Kulipiwa ada hadi 100% kwa baadhi ya programu za Shahada, Shahada ya Uzamili, au Shahada ya Uzamivu katika VCU.
“Cheti cha Kocha wa Maisha na Biashara kitakachotolewa baada ya kuhitimu ili kuimarisha ujuzi wa uongozi na ujasiriamali.
Pia ameongeza Wapokeaji wa ufadhili pia watalazimika kushiriki katika hafla moja ya mahafali ya kimataifa ya VCU itakayofanyika:Mei 23, 2026, au Oktoba 18, 2026, hapa Tanzania.
Amefafanua kuwa Mwombaji anatakiwa kuwa na kigezo vya kustahiki, Ili kuhitimu, waombaji lazima:
Wawe raia wa moja ya nchi tano zinazoshiriki.
“Wamiliki cheti cha kidato cha nne/sita (kwa shahada ya kwanza) au shahada ya kwanza (kwa shahada ya uzamili/uzamivu). “Waonyeshe uhitaji wa kifedha na kutoweza kujigharamia masomo yao kikamilifu.
“Wajitolee kumaliza programu, miradi ya kijamii, na cheti cha kocha wa maisha na biashara cha VCU.
“Wamiliki ufahamu mzuri wa lugha ya Kiingereza na upatikanaji wa mtandao wa uhakika kwa ajili ya masomo ya mtandaoni. Mwaombaji wanapaswa kuwasilisha: Fomu ya maombi mtandaoni, CV (Wasifu binafsi), Barua binafsi.
“Uwezo wa uongozi, Umahiri wa kitaaluma,Ulinganifu na dhamira ya VCU ya kuunganisha imani na elimu ili kuzalisha viongozi wa maadili, huruma, na maono.
image quote pre code