Tatizo la Uvimbe kwenye ubongo chanzo,dalili na Tiba
Uvimbe kwenye ubongo (brain tumor) ni hali ambayo seli hukua kwa wingi na bila kudhibitiwa ndani ya ubongo. Uvimbe huu unaweza kuwa wa asili ya saratani (malignant) au usio na saratani (benign) lakini aina zote zinaweza kusababisha madhara kwa sababu ubongo una nafasi ndogo ndani ya fuvu, hivyo kitu chochote kinachoongeza presha kinaweza kuathiri kazi zake.
Sababu zinazoweza kuchangia
- Kurithi vinasaba fulani (genetic mutations).
- Mionzi ya muda mrefu kwenye kichwa.
- Magonjwa fulani ya kurithi kama Li-Fraumeni syndrome, Turcot syndrome.
- Mambo yasiyoelezeka wazi – Hapa mara nyingi chanzo hakijulikani wazi.
Dalili kuu
Dalili hutegemea ukubwa na eneo la uvimbe, lakini mara nyingi ni:
- Kichwa kuuma sana,hali inayoendelea, hasa asubuhi.
- Kichefuchefu na kutapika bila kuwa na shida ya tumbo.
- Mabadiliko kwenye kuona (kama kuona mara mbili, kupoteza sehemu ya uono).
- Kizunguzungu au kupoteza balance ya mwili.
- Degedege (seizures).
- Udhaifu upande mmoja wa mwili.
- Mabadiliko ya tabia au kupoteza kumbukumbu.
- Uchovu usioelezeka.
Aina za uvimbe wa ubongo
- Benign tumors: meningioma, pituitary adenoma.
- Malignant tumors: glioblastoma, astrocytoma, medulloblastoma.
- Metastatic tumors: saratani kutoka sehemu nyingine ya mwili kuenea kwenye ubongo (mfano mapafu, matiti).
Uchunguzi
- CT scan au MRI ya kichwa.
- EEG kama kuna degedege.
- Biopsy (kipande kidogo cha uvimbe kuangaliwa maabara).
Matibabu
Hutegemea aina, ukubwa na eneo:
- Upasuaji (kuondoa uvimbe).
- Radiotherapy (mionzi).
- Chemotherapy (dawa za saratani).
- Targeted therapy au immunotherapy kwa baadhi ya aina.
- Dawa za kusaidia dalili (kama jamii ya steroids kupunguza uvimbe, dawa za degedege)n.k.
Muhimu: Uvimbe kwenye ubongo ni tatizo kubwa linalohitaji uchunguzi na matibabu ya haraka hospitalini chini ya daktari bingwa wa magonjwa ya neva au upasuaji wa ubongo.
image quote pre code