TUKIO:Miili Mitano yagunduliwa nchini Kenya kwenye kijiji kimoja

TUKIO:Miili Mitano yagunduliwa nchini Kenya kwenye kijiji kimoja

#1

TUKIO:Miili mitano yagunduliwa nchini Kenya kwenye kijiji kimoja



Takribani miili mitano ikiwemo ya watoto wawili, imefukuliwa katika kijiji cha Kwa Binzaro kaunti ya Kilifi, pwani ya kaskazini mwa Kenya, katika eneo linalohusishwa na mauaji ya Shakahola yaliyoishitua dunia mwaka 2023.

Uchunguzi wa awali umeonesha kuwa baadhi ya miili hiyo imezikwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita. 

Wakati huo huo, watu 11 wamekamatwa, watatu kati yao wakitambuliwa kama waathirika. Daktari wa serikali wa uchunguzi wa maiti Dkt. Richard Njoroge, anaeleza kuhusu shughuli hiyo ya uchunguzi.

“Leo tumeanza mchakato wa kufukua miili ya sehemu zinazodhaniwa kuwa ni makaburi hapa kwenye kijiji cha Kwa Binzaro. Mwanzoni mwa shughuli hii tulikuwa na maeneo 27 yanayodhaniwa kuwa ni makaburi. Leo tumefanikiwa kuyafukua sita.

Kati ya hayo tumepata miili mitano. Pia katika eneo hili tumepata viungo 10 vya mwili vilivyotapakaa kwenye sehemu mbalimbali ardhini. 

Mnamo mwezi Julai, ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma ya Kenya ilisema inaamini wahanga waliozikwa Shakahola walilazimishwa kufunga kutokana na kushiriki na kuamini itikadi kali za kidini. Source:Dw.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code