Tumia njia hizi kugundua ugonjwa wa figo,dalili hizi zitakujulisha
Figo hufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja katika mwili wetu. Huondoa taka katika mwili. Kuweka uzaini wa maji na madini ya elektroliti.
Figo hufuatilia shinikizo la damu na pia kusaidia katika kutengeneza seli nyekundu za damu. Lakini mara nyingi watu hupuuza dalili za mwanzo za figo kushindwa kufanya kazi vizuri.
Ikiwa ishara hizi zitatambuliwa kwa wakati, matibabu ya magonjwa yanayohusiana na figo yanaweza pia kuanza mapema.
Tutazame dalili tano za tatizo la figo. Hizi zinaweza kuwa ishara za ugonjwa wa figo na tatizo la figo.
Mkojo
Kukojoa mara kwa mara kunaweza kuwa ishara ya figo kushindwa kufanya kazi vizuri.
Mara nyingi, mkojo wenye povu ndio huelezwa kuwa ishara ya tatizo la ani.
Lakini hilo sio jambo pekee, anasema Dk Mohsin Wali, mshauri mkuu katika Hospitali ya Sir Gangaram. Magonjwa mengine pia yanaweza kusababisha povu kwenye mkojo.
Kuvimba mwilini
Kuvimba kwa macho na miguu inaweza kuwa ishara ya kushindwa kwa figo kufanya kazi vyema. Ikiwa kuna uvimbe kwenye vifundo na msuli wa nyuma ya mguu, hilo halipaswi kupuuzwa. Ni dalili ya ugonjwa wa figo.
Dk. Garima Agarwal, Mtaalamu Mshauri wa figo katika Hospitali ya Manipal, anasema, mtu anapaswa kuwa mwangalifu wa miguu inapovimba. Kuvimba kwa macho, uso na miguu ni dalili ya ugonjwa wa figo.
Shinikizo la damu
Kulingana na wataalamu, shinikizo la damu ni upanga wenye ncha mbili. Shinikizo la damu huathiri figo.
Kwa kuongezea, shinikizo la damu huongezeka hatari ya figo kushindwa kufanya kazi.
Kwa hiyo, mtu anapaswa kuwa macho kuhusu shinikizo la damu.
Ugonjwa wa kisukari
Figo huathirika zaidi kutokana na ugonjwa wa kisukari.
Dk Garima Agarwal anasema asilimia 80 ya wagonjwa wa figo wanaugua kisukari.
Katika asilimia 30 hadi 40 ya kesi za kisukari, figo huathiriwa.
Ugonjwa wa figo huanza kukua kutokana na viwango vya juu vya sukari kwa miaka mingi.
Uchovu, kuwashwa na kichefuchefu
Uchovu, kuwashwa katika mwili na kichefuchefu vinaweza kuwa dalili za ugonjwa wa figo.
Kulingana na wataalamu, kuwashwa husababishwa na ukosefu wa madini ya fosforasi katika mwili. Ugonjwa wa figo husababisha upungufu wa fosforasi katika mwili.
Baadhi ya wagonjwa wenye ugonjwa wa figo huanza kuhisi kichefuchefu. Hawajisikii kula.
Wataalamu wanasema kuishi kwa kuzingatia mtindo wa masiha wenye afya, husaidia sana katika kuzuia magonjwa ya figo. Wanasema mazoezi ya mara kwa mara, kunywa maji ya kutosha na kutumia chumvi kidogo na sukari kidogo kunasaidia katika kuzuia magonjwa ya figo.
Njia za kuhifadhi figo
Kunywa maji ya kutosha
Maji yana jukumu muhimu katika afya ya figo. Unapokunywa maji ya kutosha, figo hutoa mkojo wa kutosha ili kuondoa vitu vyenye madhara katika mwili mwili.
Pia, hatari ya mawe ya figo na maambukizi hupungua. Ikiwa unakunywa maji ya kutosha, mkojo wako utakuwa mweupe au wa njano nyepesi.
Dk Garima Aggarwal anasema, kwa ujumla mtu anapaswa kunywa lita mbili hadi mbili na nusu za maji kwa siku.
Kula chumvi kidogo
Chumvi iliyozidi si nzuri kwa figo kwa sababu huongeza shinikizo la damu na kuharibu figo. Epuka vyakula vya kusindikwa wenye chumvi nyingi.
Siku hizi, mtindo wa matumizi ya chumvi ya mawe umeongezeka. Lakini wagonjwa wa shinikizo la damu hawapaswi kula chumvi ya mawe.
Dk. Mohsin Wali anasema kwa ujumla inaaminika kuwa chumvi ya mawe ni bora zaidi kwa afya kuliko chumvi ya kawaida. Lakini ina potasiamu kidogo na sodiamu nyingi.
Punguza sukari
Ikiwa unataka kuepuka magonjwa ya figo, kula sukari kidogo.
Ni bora kutokula sukari. Vitu kama keki, biskuti, zina sukari iliyochakatwa. Sukari huongeza unene na huongeza hatari ya ugonjwa wa figo.
Uzito mdogo wa mwili
Wataalamu wanasema unapaswa kupunguza uzito kwa sababu watu wanene wako kwenye hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa figo.
Fanya mazoezi mepesi ya mwili. Ni muhimu sana. Mazoezi yataiweka metaboliki kuwa nzuri.
Na unapofikia umri wa miaka 50, hatari ya ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu itapungua.
Kula mlo kamili
Kula lishe yenye matunda, mboga mboga, na nafaka nzima. Epuka kula vyakula vya kukaanga.
Unywaji wa kutosha wa maji, ulaji wa lishe bora na mazoezi hufanya figo kuwa na afya na afya yako kwa ujumla inabaki kuwa nzuri.
Usile dawa bila ushauri wa daktari
Dk. Garima Aggarwal anasema, “Mara nyingi tunaona watu wananunua dawa kutoka duka la dawa na kuzitumia bila kushauriana na daktari.
Dk. Garima Aggarwal anasema watu wengi hutumia dawa za kutuliza maumivu.
Kulingana na yeye, "Wazee mara nyingi huchukua dawa za kutuliza maumivu ya mwili na ugonjwa wa mifupa. Dawa zingine zinaweza kuharibu figo." via Bbc.
image quote pre code