Habari za Leo Mtu wa Mungu,Ujumbe wa Leo kwako-USIOGOPE,simama tu(Imarisha imani yako kwa Mungu) ukauone wokovu wa Bwana atakaokufanyia leo; kwa maana hao Wamisri uliowaona leo hutawaona tena milele KWA JINA LA YESU.
Wamisiri;wanaweza kuwa adui zako,Magonjwa yanayokusumbua,chochote ambacho unaona kimesimama mbele yako kama mlima(vyote hivi hutaviona tena kuanzia Leo)
Bwana atakupigania wewe,nawe utanyamaza kimya. Haijalishi adui wako wangapi,hata kama wamekuja na magari 600,pamoja na Farasi zao,na kila aina ya Silaha;USIOGOPE,Bwana atakupigania wewe,na hao madui hutawaona tena Milele.
(Soma Kutoka 14:13-14). "Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa Bwana atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele. Bwana atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya".
image quote pre code