Warioba: SUA muhimu kwa maendeleo Tanzania
MOROGORO: MKUU wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba amesema amekuwa na mvuto maalum kwenye kilimo tangu awali kutokana na malengo ya Serikali yaliyowekwa juu ya kuondoa umaskini.
Jaji Warioba alisema hayo wakati wa halfa ya mkutano maalum wa Baraza la Chuo la kuanga Baraza la Chuo kwa Tathlitha ya 13 ambalo limemaliza na muda wake chini ya Mwenyekiti Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman na kulikaribisha Baraza jipya la Chuo kwa Tathlitha ya 14.
Jaji Warioba alisema alipokuwa katika uongozi na hasa kwenye nafasi ya Waziri mkuu alivutiwa zaidi na kilimo hasa kutokana na nafasi yake hiyo kusikia mambo mengi ikiwa na kusimamia kila sekta.
“ Nilipokuwa na nafasi hivyo , nilikuwa na mvuto maalumu wa kilimo kutokana na yale malengo tuliyokuwa nayo ambalo moja ni kuondoa umaskini na kwamba huwezi kuondoa umaskini mpaka umeendeleza kilimo,”alisema Jaji Warioba .
Jaji Warioba alisema alipokuwa katika nafasi hiyo alikuwa akisumbua watu wa Vyuo juu ya kilimo na kwamba wakati huo Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kilikuwa kimeanza na hakuwa akipata matunda (wataalamu) kutoka katika Chuo Kikuu hicho.
“ Nilikuwa ninatumia watu wengi ili wanipe ushauri juu ya namna gani tunaweza kuendeleza kilimo “ alisema Jaji Warioba
Jaji Warioba alisema wakati alipostaafu nafasi ya Waziri Mkuu na ilipofika mwaka 2016 Rais Dk John Pombe Magufuli alimteua kuwa mkuu wa Chuo Kikuu SUA .
“ Kwa kweli nilifurahi na si kwamba ni kuja mahali hapa ,isipokuwa nilikuwa na ile interest yangu ( Mvuto) ya mambo ya kilimo , nimekuja SUA na nimekaa huu ni mwaka wangu wa tisa “ alisema Jaji Warioba.
Alisema , SUA ina muhimu zaidi kwa maendeleo ya Tanzania ,kwani kimeendelea kufanya kazi kubwa zaidi na si kutoa ya mafunzo pekee na utafiti bali ni chachu ya elimu ya kujitegemea kwa wahitimu.
“ SUA imepiga hatua kubwa , si tu katika mafunzo na utafiti, bali pia katika maboresho ya mazingira ya kujifunzia na kufanya kazi ingawa rasilimali zetu ni chache, tumepata matokeo makubwa kupitia usimamizi makini wa Baraza,” alisema ,Jaji Warioba.
Naye Mwenyekiti Mpya wa Baraza la Chuo kwa Tathlitha ya 14 Andrew Massawe , alimpongeza Jaji Mkuu Mstaafu Chande kwa mchango wake mkubwa katika kuimarisha SUA na kuahidi kuendeleza kazi nzuri iliyoachwa.
“Katika zama hizi za sayansi na teknolojia, tunahitaji ubunifu, mshikamano, na matumizi bora ya rasilimali ili kuhakikisha SUA inabaki kinara wa ubora kitaifa na kimataifa,” alisema Massawe.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho, Profesa Raphael Chibuda licha ya kumshukuru Jaji Mkuu Mstaafu Chande kwa uongozi wa mfano na kuwatambua wajumbe wote wa Baraza lililopita, kwa msaada mkubwa katika masuala ya ushauri na uratibu na wizara husika.
Profesa Chibunda alisema kuwa nguvu mpya kutoka Baraza jipya zinapaswa kuunganishwa na uzoefu wa wajumbe waliopo ili kuiwezesha SUA kusonga mbele.
“Chuo kimepanga kuendeleza nafasi yake kama kitovu cha elimu, utafiti, na ubunifu kwa maendeleo endelevu ya taifa” alisema Profesa Chibunda.
image quote pre code