Wingu moja lina uzito Sawa na Msafara wa tembo 80 wa Kiafrika
Ingawa linaonekana jepesi na linaloelea angani kama pamba, wingu la kawaida la aina ya cumulus linaweza kuwa na uzito wa takribani tani 500 sawa na msafara wa tembo 80 wa Kiafrika.
Kwa mujibu wa National Center for Atmospheric Research (NCAR), wingu lina mamilioni ya matone madogo ya maji au chembe za barafu. Kila tone ni dogo kiasi cha kutoweza kuhisi uzito wake, lakini yanapojumlishwa yote, uzito wake unakuwa mkubwa ajabu.
Licha ya kuwa zito kiasi hiki, mawingu hubaki yakielea juu ya anga kwa sababu hewa yenye joto inayopanda juu (updraft) inayaweka hewani, na ukubwa mdogo wa matone ya maji unayafanya yasishuke chini haraka.
image quote pre code