Breaking:Ndege Ya Mizigo Ya Emirates Yatumbukia Baharini Hong Kong, Watu Wawili Wafariki

Breaking:Ndege Ya Mizigo Ya Emirates Yatumbukia Baharini Hong Kong, Watu Wawili Wafariki

#1

Breaking:Ndege Ya Mizigo Ya Emirates Yatumbukia Baharini Hong Kong, Watu Wawili Wafariki

Ndege ya mizigo iliyokuwa ikielekea kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hong Kong imepoteza mwelekeo na kutumbukia baharini leo alfajiri.

Kwa mujibu wa mamlaka za usafiri wa anga, ndege hiyo aina ya Boeing 747-400(BDSF) ilikuwa ikiendeshwa na ACT Airlines kwa niaba ya Emirates SkyCargo, na ilitoka Uturuki kabla ya kufika Hong Kong.

Taarifa zinaeleza kuwa ndege hiyo ilipokuwa ikitua kwenye njia ya kaskazini, iligonga gari la huduma lililokuwa karibu na njia ya kurukia, na kugonga kwa nguvu kulisababisha gurudumu moja kung’oka na kuwarusha abiria waliokuwa ndani ya ndege kuelekea baharini.

Ndege iliteleza kushoto nje ya njia ya kurukia takribani futi 5,000 kutoka kwenye mwanzo wa njia hiyo, ikiwa na kasi ya takriban knot 90 juu ya ardhi, na kuishia kuelekea ukuta wa baharini.

Watu wawili waliokuwa kwenye gari la huduma waliripotiwa kufariki dunia huku Wafanyakazi wanne waliokuwa ndani ya Ndege hiyo wakinusurika katika ajali hiyo.

Uwanja wa ndege umefunga kwa muda njia moja ya kurukia ndege ili kuruhusu shughuli za uokoaji na uchunguzi kuendelea.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code