Idadi ya vifo vilivyotokana na kimbunga Melissa kilichopiga mataifa ya Karibea imeongezeka

Idadi ya vifo vilivyotokana na kimbunga Melissa kilichopiga mataifa ya Karibea imeongezeka

#1

Idadi ya vifo vilivyotokana na kimbunga Melissa kilichopiga mataifa ya Karibea imeongezeka. Kimbunga hicho kimewaua watu nane nchini Jamaica na watu wasiopungua ishirini na tano nchini Haiti.

Wakati jitihada za uokozi zikiendelea, Kituo cha Kitaifa cha Marekani kinachoshughulikia vimbunga kimetoa tahadhari kwamba huenda kukawa na ongezeko kubwa zaidi la dhoruba katika maeneo hayo.

Kimbunga Melissa kinatajwa kuwa ni kibaya zaidi kuwahi kutokea tangu kuanza kuwekwa kwa rekodi za vimbunga miaka 174 iliyopita katika maeneo hayo. 

Inaelezwa kwamba kimbunga hicho kimeiacha asilimia sabini na saba ya kisiwa cha Jamaica bila ya umeme.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code