Je, Paracetamol husababisha usonji? fahamu hapa

Je, Paracetamol husababisha usonji? fahamu hapa

#1

 Je, Paracetamol husababisha usonji?

Mnamo Aprili, Waziri wa Afya na Huduma za Kibinadamu wa Marekani, Robert Kennedy Jr., aliahidi kuanzisha mpango mkubwa wa uchunguzi na utafiti wa kisayansi kwa lengo la kubaini chanzo cha ugonjwa wa usonji ndani ya kipindi cha miezi mitano.

Hata hivyo, wataalamu wengi wanatahadharisha kuwa kugundua chanzo kamili cha usonji si jambo rahisi, kwani ni hali tata ambayo imekuwa ikifanyiwa utafiti kwa miongo kadhaa.

Mtazamo wa sasa miongoni mwa watafiti ni kuwa:

"Usonji haina chanzo kimoja maalum, bali ni matokeo ya mwingiliano wa sababu za kijenetiki na mazingira."

Mnamo Agosti, mapitio ya kitaalamu yaliyoongozwa na Mkuu wa Shule ya Afya ya Umma ya Chuo Kikuu cha Harvard yalibainisha kuwa watoto wanaweza kuwa katika hatari kubwa zaidi ya kupata usonji na matatizo mengine ya maendeleo ya ubongo ikiwa walikuwa wameathiriwa na paracetamol wakati wa ujauzito.

Hata hivyo, utafiti mwingine uliochapishwa mwaka 2024 haukuonesha uhusiano wowote kati ya matumizi ya Tylenol (jina la kibiashara la paracetamol) na usonji.

"Hakuna ushahidi madhubuti au utafiti wa kuaminika unaothibitisha uhusiano wa kisababishi," alisema Profesa Monique Botha, mtaalamu wa saikolojia ya kijamii na maendeleo kutoka Chuo Kikuu cha Durham.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code