Jinsi ya kutambua dalili za mshituko wa moyo

Jinsi ya kutambua dalili za mshituko wa moyo

#1

Jinsi ya kutambua dalili za mshituko wa moyo



Dalili tofauti hutokea kwa watu tofauti, lakini ya kawaida ni maumivu ya kifua sio tu maumivu makali, bali mashinikizo au kubanwa sana kifuani.

Kwa wanawake, maumivu ya kifua yanaweza kuambatana na maumivu kwenye shingo, mikono yote miwili, mgongo au taya.

Dkt. Ailin Barseghian, daktari wa moyo kutoka California, anasema:

"Wakati mwingine, watu huchanganya mshituko wa moyo na kiungulia (indigestion). Lakini tofauti ni kuwa, maumivu ya mshituko wa moyo husambaa hadi mkono wa kushoto, taya, mgongo au tumbo."

Dalili nyingine ni:

  • Kuhisi kizunguzungu au kudhoofika
  • Kutokwa jasho kupita kiasi
  • Kupumua kwa shida au kwa sauti (wheezing)

Wakati mwingine dalili huanza masaa au siku kabla ya tukio. Ikiwa una maumivu ya kifua yasiyopungua kwa kupumzika hiyo ni ishara ya hatari.

Dkt. Barseghian anashauri:

"Baada ya saa tatu, misuli ya moyo huanza kufa. Tumia tembe ya aspirini huku ukisubiri huduma ya dharura."

Madaktari wa moyo wanasisitiza kupata matibabu mara moja ikiwa unafikiri unaweza kuwa na mshtuko wa moyo.

"Jua hali yako: umri, uzito, historia ya familia, kama unavuta sigara au unakunywa pombe. Ukiona dalili, hasa shinikizo kifuani, piga simu kwa huduma ya dharura mara moja." Usisite. Daktari Levine anasema.

Watafiti wameonya kuwa magonjwa ya moyo mara nyingi huchukuliwa kama 'magonjwa ya wanaume', jambo linalosababisha wanawake kutoshirikishwa vya kutosha katika tafiti na hivyo kutopata matibabu bora kwao.

Utafiti uliohusisha watu karibu 300,000 nchini Uingereza, ulionyesha wanawake, watu weusi, na wanaoishi katika mazingira duni, walikuwa na nafasi ndogo ya kufanyiwa upasuaji wa moyo, na walikufa au kurudi hospitalini ndani ya mwaka mmoja baada ya upasuaji.

Vitu kama shinikizo la damu, uvutaji sigara, na kisukari huongeza hatari kwa wanawake zaidi kuliko wanaume.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code