Mwanariadha mahiri wa Tanzania, Simbualphonce , anaendelea kuipeperusha vyema bendera ya taifa

Mwanariadha mahiri wa Tanzania, Simbualphonce , anaendelea kuipeperusha vyema bendera ya taifa

#1

Mwanariadha mahiri wa Tanzania, Simbualphonce , anaendelea kuipeperusha vyema bendera ya taifa baada ya kutajwa rasmi miongoni mwa wanaowania tuzo ya kimataifa ya “Out of Stadium Athlete of the Year” katika World Athletics Awards 2025, mojawapo ya tuzo kubwa zaidi duniani kwa wanariadha.



Uteuzi huu wa kihistoria unakuja kufuatia mafanikio makubwa ya Simbu katika mbio ndefu mwaka huu, ambapo amethibitisha ubora wake kwa kutwaa medali ya dhahabu katika mashindano ya World Athletics Championships. Ushindi huo ulimuweka kwenye ramani ya dunia kama mmoja wa wanariadha bora zaidi wa kizazi chake.

Simbu sasa anachuana na majina makubwa katika dunia ya riadha akiwemo Caio Bonfim kutoka Brazil, Evan Dunfee wa Canada, Yomif Kejelcha kutoka Ethiopia, na Sabastian Sawe wa Kenya wote wakiwa wanariadha wenye rekodi kubwa katika mashindano ya kimataifa.

Tuzo hizi hutolewa kila mwaka na World Athletics kwa lengo la kutambua na kupongeza wanariadha waliofanya vizuri zaidi duniani katika mwaka husika. Sherehe ya utoaji wa tuzo hizo inatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu mjini Monaco.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code